NJOHOLE LEGEND FOUNDATION CHACHU YA SOKA BONGO

 MCHEZAJI wa Kimataifa Renatus Njohole Juzi usiku amefungua ukurasa mpya kwa wanamichezo wa soka nchini kwa kuzindua mfuko wake utajaofahamika kwa jina la Njohole Foundation.
Uzinduzi huo uliofana ulifanyika kwenye Hoteli ya Movenpick  Jijini Dar es Salaa na kushuhudiwa na wanamichezo kadhaa wakiwemo familia ya Njohole , Sunday Manara, Juma Pondalami nawengineo wengi.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Naibu wa Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juliana Yasoda amesema wao kama serikali nafsi zinawasuta wanapowaona wachezaji wa zamani wanataabika mitaani wakiwa hawana mbele wa nyuma.
Akizungumza Dar es Salaam juzi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Michezo, Leonard Thadeo katika uzinduzi wa Njohole Legend Foundation ambayo lengo lake ni kusaidia wachezaji wa zamani, Yasoda alisema familia ya Njohole imefanya kitu kizuri kuwakumbuka wachezaji hao hivyo seriali itahakikisha jambo hilo linafanikiwa.


"Kwa kweli naipongeza Njohole Foundation kwa kuanzia jambo hili sisi tutahakikisha serikali inalisimamia jambo hili na kufanikiwa licha ya kwamba kwa sasa lipo katika makaratasi," alisema Yasoda.
Alisema mfuko huo umekuja kwa wakati na kuwataka wadau wengine waige mfano huo kwani ni kweli wachezaji waliowika zamani wamekuwa wakitaabika wakati wao ndiyo chachu ya kukuza michezo kwa vijana wadogo.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Idd Kipingu familia ya Njohole imeanzisha daraja la kurithishana kwani wachezaji wa zamani ni njia ya kwenda katika mafanikio kwani wao katika enzi zao walifanikiwa tofauti na sasa.
"Miaka ya 1960 hadi miaka 1980 mwishoni timu zetu za Simba na Yanga zilikuwa zikifanya vyema tofauti na sasa na siri ya wachezaji wa zamani waliwa wanaweza kujichunga wenyewe tofauti na wachezaji wa sasa wambao wanawekwa kambini na kulindwa wasitoroke.
"Kwa kweli kuna tofauti kubwa kati ya wachezaji wa zamani na wa sasa ambao wanakula chips mayai chakula ambacho hakina nguvu mwilini, lakini zamani wachezaji walikuwa wakila ugali na maharage," alisema.
Mwenyekiti wa Njohole Foundation, Renatus Njohole ambaye aliwahi kuichezea Simba na sasa anacheza soka la kulipwa nchini Uswis alisema lengo lao ni kutaka kuwasaidia wachezaji wa zamani kwa kuwapa mikopo na kuwainua kimaisha.
Alisema ameamua kuanzisha mfuko huo kwa kuwa wachezaji wa zamani kwa kiasi kikubwa ndiyo wamewafanya wao kupata mafanikio kwa kuwa walipokuwa wadogo walihakikisha wanacheza soka kwa bidii ili kufikia viwango vya wachezaji hao.
"Kwa kuwathamini wachezaji wa zamani ni njia mojawapo ya kuhamasisha wachezaji chipukizi kujikita katika michezo mbalimbali na si soka peke yake ndiyo maana leo (juzi), tumealika wachezaji wa michezo tofauti," alisema Njohole.
 Renatus  Njohole Kushoto akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Luteni Kanali Mataafu Idd Kipingu.
 Mwenyekiti wa Njohole Legend Foundation , Renatus Njohole  akiwa na Mwenyekiti wa BMT Kipingu.
 Njohole kushoto akiwa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Michezo Juliana Matagi Yassoda.
 Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano Kampuni ya Bia ya Serengeti Teddy Mapunda, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Michezo Juliana Matagi Yassoda, Msaidizi wa Msaidizi wa Mkurugenzi wa Mahusiano Nandi Mwiyombela na Mkuu wa Mambo ya Ndani SBL Imani Lwinga.
 Mkurugenzi wa Njohole  Legend Foundation, Renatus Njohole akizungumza mbele ya wadau.
 Baadhi ya wadau wakiwa katika tukio hilo katika Hoteli ya Movenpick.
 MC wa shughuli hiyo,Ephrain  Kibonde.

 Wakurugenzi  wakijadili jambo.
John Mwansansu mwenye Suti  akiwa na washkaji.

Post a Comment

0 Comments