UMAARUFU CHANZO CHA WASANII KUPATA MAAMBUKIZI YA VVU: BASATA

Katikatini Muelimishaji rika Taji Liundi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirikikala Utangazatila Taifa (TBC International) akitoa elimu kwa wasanii na wadau wa Sanaa juu yaVVU/UKIMWI wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA).Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego na Mratibuwa Jukwaa hilo Ruyembe C.Mulimba.


TajiLiundi akiwaonesha wadau wa Jukwaa la Sanaa moja ya wasanii aliyefariki Duniakutokana na kupata maambukizi ya VVU/UKIMWI.Alitoa mifano ya wasanii mbalimbaliwaliokwisha fariki kutokana na ugonjwa huu.


KatibuMtendaji wa BASATA,Bw.Materego akitoa wito kwa wasanii kushiriki katikakujikinga na VVU/UKIMWI kwenye Jukwaa la Sanaa linaloandaliwa na Baraza hilokila Jumatatu kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa naUtamaduni (CAJAtz).Kushoto kwake ni Taji Liundi na Bw.Ruyembe.

Mdauwa Jukwaa la Sanaa akiuliza swali kuhusu VVU/UKIMWI Wadauwengi wa sanaa humiminika kwenye Jukwaa la Sanaa kupata elimu na changamotombalimbali kuhusu tasnia.Hapa wadau wakifuatilia somo la VVU/UKIMWI kwa umakinimkubwa.




Na Mwandishi Wetu




Wasanii wametajwa kuwa hatarini kuambukizwa virusi vya UKIMWIkutokana na umaarufu walionao na kujikuta wakishawishika kuingia katika vitendombalimbali vya hatari kwa afya zao hasa vya ngono.




Hayo yamesemwa wiki hii na Muelimisha rika Taji Liundi wakatiakiwasilisha mada kuhusu Umuhimu wa Msanii Kutunza Afya Yake kwenye Jukwaa laSanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) ambapo alisema kwamba, umaarufu, ushawishi na kutojitambua miongonimwao ndiyo chanzo kikubwa cha wao kuwa hatarini kupata maambukizi hayo.




“Kutojitambua, umaarufu na ushawishi mkubwa walionao wasaniikatika jamii huwafanya wawe hatarini kuathiriwa na ugonjwa wa UKIMWI kwanihufuatwa na kundi la watu na mara nyingi kujikuta wakishawishiwa kufanya ngonokatika mazingira yasiyo salama” alisema Taji Liundi ambaye ni Kamishna msataafuwa Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS).




Aliongeza kwamba,kada ya wasanii imekuwa ikiathiriwa naugonjwa huu toka umegunduliwa kwani katika nchi zilizoendelea kumekuwa nataarifa za vifo vya wasanii wengi vinavyotokana na UKIMWI huku akiweka wazikwamba kutumia vibaya umaarufu ambako kumekuwa kukichanganywa namatumizi ya vilevini sababu nyingine kuu.




Alizidi kueleza kwamba,uwepo wa tunzi za kimapenzi katikakazi za sanaa ni changamoto nyingine kwani imezifanya kazi za wasanii kuwa zakusisimua na kuamsha utendaji ngono miongoni mwa wanajamii na kuwaacha waowakiwa waathirika wakubwa.




“Ukitazama nyimbo za wasanii wa kizazi kipya utaona ni zenyemaudhui ya rika la adolescence (umri wa makumi),zimebeba ujumbe wenyekuhamasisha mapenzi na ngono na hapa ndipo tunapoona mabadiliko makubwa yavijana wakihamasika kufanya yale wanayoyaona na kuyasikia kupitiavyombo vya habari”alisisitiza Taji.




Alimalizia kwa kuwaasa wasanii kujitambua, kujilinda nakuwajibika katika kupambana na VVU/UKIMWI huku akiwaeleza kwamba,umaarufu naushawishi walionao huathiriana na jamii (Two way effects) hivyohawana budi kuwa makini.




Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materegoalisema kwamba, wasanii wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu dhidi ya UKIMWIkwa jamii na kujisahau wao binafsi kwamba wako katika mazingira hatari yakupata maambukizi.




Alisema kwamba,BASATA katika mpango mkakati wake wa 2011-2014itajikita katika kutoa elimu kwa wasanii na kuwapa ufahamu juu ya ugonjwa huuhatari ambao umekuwa ukiwaua wasanii mbalimbali duniani.

Post a Comment

0 Comments