Kocha Jamhuri Kihwelo ameongeza wachezaji saba kwenye kikosi chake cha U23 kwa ajili ya mechi ya marudiano ya mchujo ya michuano ya Olimpiki dhidi ya Cameroon itakayochezwa Jumamosi (Aprili 9 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Wachezaji hao ni Kigi Makasi kutoka Yanga, David Luhende (Kagera Sugar), Jabir Aziz (Azam), Kelvin Chale (Simba), Ali Lundenga (Kagera Sugar), Mrisho Ngasa (Azam) na Juma Abdul (Mtibwa Sugar). VIINGILIO U23 v CAMEROON
Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni kuanzia sh. 1,000. Mashabiki watakaokaa viti vya kijani, bluu na rangi ya chungwa (orange) ndiyo watakaolipa kiasi hicho wakati VIP B na VIP C kiingilio kitakuwa sh. 5,000. Jukwaa la VIP A lenye viti 745 kiingilio kitakuwa sh. 10,000. Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo na siku yenyewe ya mechi. Tiketi zitauzwa katika vituo vya OilCom Ubungo, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Samora/Ohio, Bigbon Msimbazi (Kariakoo) na Uwanja wa Uhuru. Mechi itaanza saa 10 kamili. Cameroon imewasili nchini jana saa 5.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways ikiwa na wachezaji 23 na imefikia Paradise City Hotel. Mwamuzi wa mechi hiyo ni Aime Ndayisenga akisaidiwa na Desire Gahungu, Jean-Claude Birumushahu na Athanase Niyongabo, wote kutoka Burundi. Kamishna wa mchezo huo ni Charles Masembe kutoka Uganda. FIFA YAISIMAMISHA BOSNIA-HERZEGOVINA
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) limeisimamisha Bosnia-Herzegovina kuanzia Aprili Mosi mwaka huu baada ya Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchi hiyo (FFBH) kutopitisha Katiba yake iliyofanyiwa marekebisho kwa kuzingatia matakwa ya FIFA na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ulaya (UEFA). Kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke iliyotumwa kwa wanachama wake, FFBH inapoteza haki zote ilizokuwa nazo kutokana na uanachama wake kwa Shirikisho hilo hadi hapo itakapotolewa taarifa nyingine. Kutokana na kusimamishwa huko, wanachama wote wa FIFA hawatakiwi kushirikiana na FF BH katika masuala yoyote isipokuwa yale yanayohusu mchezaji binafsi. Hatua hiyo imefikiwa kutoka na uamuzi uliofikiwa Oktoba 28 mwaka jana na Kamati ya Utendaji ya FIFA kuwa FFBH iwe imetekeleza matakwa hayo kufikia Machi 31 mwaka huu. Boniface Wambura Ofisa Habari TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIAprili 5, 2011
VIINGILIO U23 v CAMEROON VYATAJWA
Viingilio katika mechi ya marudiano ya mchujo ya michuano ya Olimpiki kati yatimu ya Taifa ya Tanzania ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 23 dhidi yaCameroon itakayochezwa Jumamosi (Aprili 9 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar esSalaam ni kuanzia sh. 1,000. Mashabiki watakaokaa viti vya kijani, bluu na rangi ya chungwa (orange) ndiyowatakaolipa sh. 1,000 wakati VIP B na VIP C kiingilio kitakuwa sh. 5,000.
Jukwaala VIP A lenye viti 745 kiingilio kitakuwa sh. 10,000. Tiketi zitaanza kuuzwasiku moja kabla ya mchezo na siku yenyewe ya mechi. Tiketi zitauzwa katika vituo vya OilCom Ubungo, Shule ya Sekondari BenjaminMkapa, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Samora/Ohio, Bigbon Msimbazi (Kariakoo)na Uwanja wa Uhuru.
Mechi itaanza saa 10 kamili. Cameroon imewasili nchini jana saa 5.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways ikiwana wachezaji 23 na imefikia Paradise City Hotel.
FIFA YAISIMAMISHA BOSNIA-HERZEGOVINA
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) limeisimamishaBosnia-Herzegovina kuanzia Aprili Mosi mwaka huu baada ya Mkutano Mkuu waShirikisho la Mpira wa Miguu la nchi hiyo (FFBH) kutopitisha Katiba yakeiliyofanyiwa marekebisho kwa kuzingatia matakwa ya FIFA na Shirikisho la Mpirawa Miguu la Ulaya (UEFA).
Kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke iliyotumwa kwawanachama wake, FFBH inapoteza haki zote ilizokuwa nazo kutokana na uanachamawake kwa Shirikisho hilo hadi hapo itakapotolewa taarifa nyingine.
Kutokana na kusimamishwa huko, wanachama wote wa FIFA hawatakiwi kushirikiana naFFBH katika masuala yoyote isipokuwa yale yanayohusu mchezaji binafsi. Hatuahiyo imefikiwa kutoka na uamuzi uliofikiwa Oktoba 28 mwaka jana na Kamati yaUtendaji ya FIFA kuwa FFBH iwe imetekeleza matakwa hayo kufikia Machi 31 mwakahuu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari.
0 Comments