Mmoja ya Wasanii waliopona kwenye ajali hiyo Ally Juma aka Ally J (Kulia) akiwa sambamba na Viongozi wa Bendi yake, Ferouz Juma (wa pili kutoka kulia) Mkurugenzi wa Bendi ya Five Star na Khamis Slim (Wa kwanza kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa Bendi. HITMA ya kuwaombea wanamuziki 13 waliokuwa wa kundi la Five Stars Modern Taarab ambao walipoteza maisha katika ajali ya gari Machi21 mkoani Morogoro, itafanyik Aprili17 kwenye ukumbi wa PTA, Temeke. Katibu wa kamati ya Hitma, Said Mdoe alisema kuwa shughuli hiyo imepangwa kuanza saa 7.00 mchana na maandalizi yake yanaendelea. Mdoe alisema kuwa wadau wote wa sanaa na burudani wanakaribishwa katika kisomo hicho pamoja na kuchangia michango yao. Alisema kuwa michango yako iwasilishwe moja kwa moja kwa mweka hazina (Ashraf Ahmed: 0713232747), au kwa Mwenyekiti (Abbas Mtemvu), Makamu mwenyekiti (Sheikh Omar Alhadi naibu imam wa msikiti wa Kichangani) au Katibu (Said Mdoe, 0713 606109) na utapatiwa stakabadhi. Pia michango hiyo inawezwa kupelekwa ofisini kwake, Kampuni ya Screen Masters iliyopo Kinondoni mtaa wa Togo. Wajumbe wengine wa kamati ni m Mhe. Idd Azan (Mbunge wa Kinondoni), Mhe. Azan Zungu (Mbunge wa Ilala), Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab Mzee Yusuf, Naibu mkurugenzi wa TOT Khadija Kopa, Asha Baraka (Mkurugenzi wa Twanga Pepeta), Hadija Shaibu “Dida” kutoka Times FM na Sakina Lioka (Clouds TV) na Mariam Migomba wa TBC. Wajumbe wengine ni pamoja na wakurugenzi wa Five Stars Modern Taarab Hamis Slim, Ali J na Feruz Juma, Mkurugengenzi wa Clouds FM Ruge Mutahaba, Abdallah Feresh (Mkurugenzi Dar Modern Taarab). Alisema kuwa kwa watu wa mikoani wanaweza wakatuma michango yao kupitia M-Pesa kwa namba 0765 111135.
WATU WATANO WAFIKISHWA MAHAKAMANI MADAI YA KUHARIBU,KUHUJUMU MIUNDOMBINU YA
RELI YA KISASA (SGR)
-
WATUHUMIWA Watano Wakiwemo Raia Wa China Wawili Wanaokabiliwa na Tuhuma
za Kuharibu Miundombinu Ya Reli Ya Kisasa (SGR) Wamepandishwa Kwa Mara
ya p...
5 hours ago
0 Comments