Social Icons

Thursday, May 21, 2015

MEMBE MGENI RASMI TAMASHA LA QASWIDA

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Qaswida lililoandaliwa na Ulamaa Promotions Centre litakalofanyika  Mei 24 kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Ustadhi Jumanne Ligopora, katika tamasha hilo, wamejipanga kushirikisha madrasa zaidi ya 50 za jijini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa.

Aidha, Ligopora alisema hivi sasa wako kwenye mchakato wa kusambaza mialiko kwa madrasa za Dar es Salaam na mikoani.

“Tunatarajia maelfu ya Waislamu kumiminika kwa wingi katika viwanja vya Benjamin Mkapa kwa lengo la kupata ladha mbalimbali za Qaswida,” alisema Ligopora.

Mwenyekiti huyo alisema wameshafanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya tamasha hilo ambalo anaamini litawapa burudani wote ambao watamwagika uwanjani hapo. 

No comments:

 
 
Blogger Templates