Social Icons

Friday, January 23, 2015

SIJASHANGAA ALLY CHOKI KUPANDA JUKWAA LA TWANGA: ASHA BARAKA


IKIWAni siku chache  tu kupita  tangu Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo Ally Choki (Wazee wa Kizigo)  pichani kulia  kupanda katika jukwaa  la bendi ya Twanga Pepeta Jumapili iliyopita katika bonanza linalofanyika  kwenye viwanja vya Leaders Club mashabiki wamponda  huku  wengine wakisifia  kitendo hicho.Wapo waliosema kwamba Choki amesambaza upendo kwa mwana mama Asha Baraka lakini wengine  Asha mwenyewe amejibu mapigo na kusema hajastushwa na kitendo hicho kwa ilivyo kwa wengine.
 
Akizungumzia jambo hilo  Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka alisema kwamba hajashangazwa na tukio hilo kwani anajua wasanii hupanda kwenye majukwaa ya bendi nyingine ikiwa ni  namna ya kusalimiana.
 
“Alipopanda jukwaani mimi sikuwepo nilikwishaondoka hivyo hiyo sehemu ya wasanii kusalimiana wenyewe kwa wenyewe , lakini pia napenda kuwaambia wasanii wawewanaweka maneno akiba kwani katika maisha kuna leo na kesho" anasema Asha.
Aisha anaendelea kwa kusema kuwa "nasema hivyo kwa sababu siku zote Choki yeye ndiye anaye zungumza hivyo mimi sitaki kuzungumza lolote zaidi ya kutolea mfano kwamba hata Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ anapaswa akumbuke walikomtoa kina Ruge Mutahaba na siku zote hakuna mabaya yanayoendelea na mtu akikukosea bora kumwita pembeni na kumweleza siyo kwenda kwenye vyombo vya habari na kuzungumza” alisema Asha.
Mwisho amewataka wasanii wote watambue kua yeye  ni mtu mzima na hata Choki ni mtumzima pia hivyo anatambua analolifanya  kwani hata katika bendi ya Twanga wote wanamuita kaka  hivyo utuuzima ni dawa  alisema Asha.
Choki alifika katika viwanja vya Leaders Club mapema jioni siku ile ambapo wasanii wa bendi ya Twanga walisikika wakisema kaka Ally kaja hivyo wakawa wakienda kumsalimia kila mmoja kwa wakati wake.

Baadaye ndipo Choki alipopanda kwenye jukwaa na kuimba wimbo wa ‘Password’ ambao ni utunzi wake Choki albamu aliyoitunga kabla  hajaipa kisogo  bendi hiyo.
 

Wakati huohuo Choki alitafutwa kwa njia ya simu simu yake ilikuwa imezimwa.

No comments:

 
 
Blogger Templates