Social Icons

Friday, January 23, 2015

MWIGULU NCHEMBA APIGIA DEBE SKAFU KUWAKILISHA UTANZANIA


NAIBU WAZIRI wa Wizara ya Fedha Mwigulu Nchemba Pichani juu amesema kwamba katika nchi ya Tanzania mchakato wa kupata vazi la taifa utakuwa mgumu kutokana na wingi wa makabila.

“Unajua Tanzania ni nchi kubwa hivyo  kutokana na wingi wa makabila yaliyomo ndani yake ni vigumu kupata vazi moja ambalo litakubalika na kila kabila huku akiwataja, wamasai, wasukuma  na wengineo hivyo ndiyo sababu akaamua  yeye  binafsi kubuni kuvaa skafu ambayo ina rangi za bendera ya nchi”alisema Nchemba.

Aliendelea kwa kusema kuwa yeye hupendelea kuvaa skafu yenye kufumwa na nyuzi za sweta kutokana na kupata msukumo kutoka kwa na baadhi ya viongozi kuwa na  mitindo ambayo iliweza kuwatambulisha  katika jamii.

“Kutokana na hilo nami nikapatwa na mguso wa kuwa navaa skafu yenye rangi za bendera ya taifa ikiwa ni njia moja wapo ya kujitambulisha vilevile skafu ni  vazi jepesi ambali linaweza kuvaliwa na mtu yeyote" anasema.

No comments:

 
 
Blogger Templates