Social Icons

Friday, January 23, 2015

OGOPA KOPA KUONGEZA LADHA TAMASHA LA CDS


KUNDI la muziki wa taarabu la Ogopa Kopa limeongezwa katika orodha ya bendi zitakazotoa burudani katika tamasha la muziki la CDS linalotarajiwa kufanyika viwanja vya TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam Januari 25.
Akizungumzia  tamasha hilo, Mratibu  Hamis Dakota pichani juu , alisema wameamua kuliongeza kundi hilo ili kuongeza ladha.

Dakota alizitaja bendi nyingine zitakazotoa burudani siku hiyo kuwa ni FM Academia, Malaika Band, Mapacha Watatu na wakongwe, Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’.

Tamasha hilo linadhaminiwa na CDS, Global Publishers na Clouds FM, ambako limepangwa kuanza saa 12 jioni kwa kiingilio cha sh. 5,000.

No comments:

 
 
Blogger Templates