Mkuu Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule Machi 30,2025 amekabidhi kwa niaba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suhulu Hassan, zawadi za mkono wa Eid kwenye vituo vya kulea watoto wenye mahitaji maalum.
Mhe.Senyamule amekabidhi zawadi hizo zilizotolewa na Mhe. Rais kwa walezi na viongozi wa vituo vya Kijiji cha Matumaini na Rahman ‘Orphanage Center ‘vilivyopo Jijini Dodoma .
“Kwa niaba ya Serikali, niendelee kuwashukuru na kuwapongeza walezi wote mnaolea watoto kwenye vituo hivi, Mungu awabariki kwa upendo mnaouonesha kwa watoto hawa” Mhe.Senyamule
Naye Kiongozi wa Kijiji cha Matumaini Padri Vicent Boselli amesema kwa zaidi ya miaka 20 kituo hicho kimekuwa kikipokea watoto wenye maambukizi ya VVU na kuwapa matumaini ya upendo na kuishukuru Serikali kwa kuwakumbuka kwenye kipindi hiki cha Sikukuu.
Kwa Upande wao Shadrack Hassan na Hazla Ramadhan ambao ni miongoni mwa watoto wenye mahitaji wanaolelewa katika vituo hivyo wamemshukuru Mhe. Rais pamoja na Uongozi wa Mkoa kwa zawadi hizo.
Zawadi zilizotolewa ni pamoja na mchele, Mbuzi, katoni za juisi, mafuta ya kupikia, unga wa sembe, maharage na mahitaji mengine muhimu.
0 Comments