"Maelekezo ya Makamu wa Rais ni Sheria maelekezo aliyotoa kwa Mamalaka ya Serikali za Mitaa ni amri msingi wake ni utekelezaji tutakapokuwa tunapita huko katika Halmashauri tutahitaji kuona inatekelezwa, Naibu Katibu Mkuu wandikie Halmashauri zote kuwa zoezi hili ni endelevu la upandaji wa miti kwa moyo wa dhati nawapongeza washiriki wote walioshiriki na kushinda kupanda miti na kukua katika kiwango cha 99% hii inaonesha kuwa ninyi ni vijana wasikivu na wema wenu nahitaji niuone katika matokeo yenu ya kidato cha nne na cha sita na nitawafuatilia", amesema Mchengerwa.
"Nawapongeza Benki ya NMB kwa kutoa uamuzi wa kutenga Mil.225 kwa ajili ya zawadi ya motisha kwa shule zilizopanda miti ambazo zimetolewa leo"amesema Mchengerwa.
Mchengerwa amesema hayo tarehe 12 Aprili 2025 alipokuwa mgeni rasmi kwenye tukio la kukabidhi zawadi kwa washindi wa Kampeni ya Miti Milioni 'Kuza mti Tukutunze' hafla iliyofanyika katika viwanja vya Sekondari ya Mwambisi Forest Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Shule ya Sekondari ya Mwambisi Forest iliyopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani imeibuka kinara kwa kupanda miti 2,000 ambayo imetunzwa kukua kwa kiwango cha 99% , kwa ushindi huo wamezawadiwa hundi yenye thamani ya Mi.50
Nafasi ya pili imekwenda kwa Shule ya Ibondo kutoka Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza ambao wamepata hundi ya Mil. 30 nafasi ya tatu imekwenda kwa Shule ya Msingi Itimbo Sekondari wamepata hundi ya Mil.20
Mchengerwa amewaomba Benki ya NMB waendelee kuchangia maendeleo ya nchi katika kushirikiana kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo nchini.
Akizungumza kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Seka Urio alikaribisha wageni na kutambulisha wahudhuriaji kwenye hafla hiyo,huku wengine waliohudhuria ni pamoja na Katibu Mkuu TAMISEMI Adolf Ndunguru, Kamishna wa Uhifadhi Wakala wa Misitu Tanzania Prof. Dos Santos, Afisa Mkuu wa Fedha Juma Kimori, Katibu Tawala Mkoa wa Pwani (RAS) Rashid Mchatta , Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon,Naibu Waziri OR-TAMISEMI (Afya) John Dugange.
Zoezi la upoandaji miti 1500 kila Mkoa lilizinduliwa mwaka 2023 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango kwenye Mji wa Kiserikali Mtumba Dodoma.
0 Comments