KISARAWE YAZINDUA MIRADI SABA YENYE THAMANI YA BIL.1.1

 

Akikagua miradi hiyo Kiongozi  wa  Mbio za Mwenge  Ussi  amesema kuwa miundombinu  ya mabomba maji  yaboreshwe kwenye mbweni la wasichana  Shule ya Kisarawe ili wanafunzi  waweze kupata huduma hiyo muhimu.



Mkimbiza  Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ussi ameweka jiwe la msiki kwenye mabweni mawili ya wasichana katika Sekondari  ya Kisarawe Mkoani Pwani leo tarehe 3 Aprili 2025.
Aidha Ussi pia amezindua miradi mingine muhimu ikiwa ni pamoja na Klabu ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iliyopo kwenye Shule ya Sekondari Kisarawe.

Aidha Ussi baada ya kukagua mabweni hayo mawili ya wasichana  ameridhika  na kusema yamejengwa kwa kuzingatia viwango na manunuzi ya Nest .

Ukaguzi wa miradi hiuo umefanyika leo tarehe 3 Aprili 2025 ikiwa ni muendelezo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru  mwaka huu.

Mradi wa Maji Kata ya Kibuta, pamoja na jengo la utawala na madarasa ya shule ya Madugike inayopatikana Manerumango.

Kwa upande wa Mradi wa Maji uliopo Kata ya Kibuta, Ussi amesisitiza kuwa wakandarasi wanatakiwa kumaliza mradi huo ndani ya wakati kama jinsi   walivyosema kuwa  wataukamilisha ifikapo Agasti mwaka huu ambapo tangi hilo maji linauwezo wa  kuhifadhi maji uwezo wa kubeba lita 90,000.

Akitolea mfano wa miradi mingine ya maendeleo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Seleman Jafo, amesema kuwa wananchi wa Kisarawe walikuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji, jambo lililosababisha serikali kuchimba kisima kirefu katika eneo hilo. Dkt. Jafo pia ametoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji unaoendelea.

"Serikali imejizatiti kuhakikisha wananchi wetu wanapata huduma ya maji kwa wakati, na leo tunashuhudia mafanikio makubwa katika mradi huu," amesema Dkt. Jafo

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, amesema kuwa ujenzi wa bweni la wasichana la shule ya Sekondari Kisarawe umegharimu zaidi ya Mil. 137  fedha za ndani.

"Bweni hili litawapa fursa wanafunzi wa kike  kusoma kwa amani na hatutakuwa na tena vikwazo vya muda mrefu wa kutembea kwa muda mrefu  jambo ambalo pia litasaidia kupunguza mimba na  ndoa za utotoni," amesema Magoti.

Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 Wilayani Kisarawe umekagua miradi yenye thamani ya zaidi ya  Bil.1 . umekimbizwa umbali wa Kilometa 195 na kukagua jumla ya miradi saba  ya maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti akicheza na Vijana wa hamasa kwenye mapokezi ya Mwenge Kiluvya Madukani. 

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti wakati akitoa taarifa wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2025 katika Wilaya ya Kisarawe ukitokea Wilayani Kibaha katika viwanja vya Kiluvya madukani ambapo katika fedha hizo ni kutoka mapato ya ndani kutoka Halmashauri ya Wilaya, kutoka Serikali Kuu, wahisani na nguvu za Wananchi.

Magoti amesema miradi itazinduliwa, mradi mmoja umewekwa  jiwe la Msingi na miradi mitatu imekaguliwa

Kiongozi wa Mbio za Mwenge  wa Uhuru  Kitaifa Ismail Alli Ussi  amezindua Miradi saba.

Akizungumzia kuhusu uchaguzi mkuu, Ussi ametoa wito kwa wananchi kujitokeza  kwa wingi kwenye uchaguzi  mkuu ujao na kupiga  kura kwa amani na kushiriki kwenye michakato ya kisiasa, ili kuchagua viongozi watakaowaongoza na kuwaletea  maendeleo.

"Ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anajihadhari na rushwa, iwe kwa kupokea au kutoa, ili tuweze kupigana nayo kwa pamoja," amesema Ussi.

Post a Comment

0 Comments