DKT. KIKWETE AWASILISHA UJUMBE WA RAIS DKT SAMIA SULUHU CONGO BRAZZAVILLE

Rais wa Awamu ya Nne na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha Ujumbe Maalum kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Congo (Congo Brazzaville), Mhe. COLLINET MAKOSSO Anatole. Mhe. Anatole amepokea ujumbe huo wa maandishi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Congo , Mhe. Denis Sassou Nguesso ambaye alikwenda Kijijini kwao kushiriki mazishi ya kaka yake.

Tukio hilo limefanyika jana tarehe 14 ,Aprili, 2025 Jijini Brazzaville kushuhudiwa na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa nchi zote mbili.

Mhe. Kikwete amewasilisha  salamu za Rais Samia ambazo zmeelezea umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kama njia muhimu kwa bara hilo kujitegemea, hususan katika kipindi hiki ambapo misaada kutoka nchi za magharibi imepungua kwa kiasi kikubwa.

Post a Comment

0 Comments