Mwenyekiti
wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), ambaye amemaliza muda
wake, Bw. Innocent Mungy, (wapili kulia), akimkabidhi nyaraka za chama, Katibu
Mkuu mpya wa chama hicho, Bw. Abdulm Njaidi. (wapili kushoto), ikiwa ni ishara
ya kukabidhi rasmi majukumu ya kiuongozi jijini Dar es Salaam Julai 20, 2017.
Wengine pichani walioshuhudia hafla hiyo ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Habari MAELEZO anayeshughulikia Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus,
(watatu kushoto), Bw. Gerald Chami, (wakwanza kushoto), ambaye ni Mweka Hazina
Msaidizi na Bw.Peter Malinzi, (kulia), Mweka Hazina aliyemaliza muda wake.
NA
MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
UONGOZI
mpya wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), umekabidhiwa rasmi
usukani wa kuongoza taasisi hiyo muhimu katika mawasiloiano ya serikali nchini.
Hafla
ya makabidhiano hayo ilifanyika jijini Dar es Salaam, Julai 20, 2017 ambapo
Mwenyekiti wa TAGCO aliyemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy, alimkabidhi “nyenzo”
za kufanyia kazi Katibu Mkuu mpya wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi, ambapo shughuli
hiyo ilishuhudiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO
anayeshuhulikia Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus, Mweka Hazina wa
chama hicho aliyemaliza muda wake, Bw.
Peter Malinzi, Mweka Hazina Msaidizi Mteule, Bw.Gerald Chami.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekliti aliyemaliza muda wake, Bw. Innocent
Mungy alisema, “tunawakabidhi TAGCO, hiki ni chombo muhimu sana kwa mawasiliano
ya serikali, hivyo hakikisheni mnakiongoza vyema ili maelengo kusudiwa yafikiwe,”.alisema
Bw. Mungy.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi alisema, “Tunashukuru kwa kukabidhiwa
usukani wa TAGCO, tunajua hiki chombo ni muhimu sana katika kuhakikisha wananchi
wanapatiwa taarifa sahihi za shughuli za Serikali yao inazofanya, tutatekeleza majukumu
yetu kwa umakini na uaminifu mkubwa, tunaomba ushirikiano kutoka kwa uongozi uliopita
na wanachama wote wa TAGCO na watendaji wote serikalini,”. Alisema Bw. Njaidi
wakati akitoa neon la shukrani.
Viongozi
wengine wapya wa TAGCO ni Bw. Pascal Shelutete (Mwenyekiti), Bi. Sarah Kibonde
Msika (Makamu Mwenyekiti), Bi. Tabu Shaibu (Mweka Hazina), Bi. Gaudensia Simwanza
(Katibu Msaidizi), Bw. Owen Mwandubya (Katibu Mwenezi) na Bw. Mpokigwa Mwakasipo
(Katibu Mwenezi Msaidizi).
TAGCO
nichama kinachowa kutanisha pamoja Maafisa Mawasiliano wa Taasisi mbambali za umma,
serikali na Halmashauri zote hapa nchini, lengo likiwa ni kupena ujuzi na uwezo
wa kuhakikisha taarifa za serikali zinawafikia wananchi kwa usahihi na kwa
wakati.

0 Comments