Mwanahabari Josephat Isango amefariki dunia leo saa moja asubuhi Mkoani Singida baada ya kuumwa kwa muda mfupi.
Marehemu Isango atakumbukwa kutokana na mchango wake mkubwa katika uandishi wa habari za siasa na jamii kwa ujumla.Nyota ya fani ya uanahabari ilishamiri alipokuwa ameajiriwa na Kampuni ya Free Media Limited ambao ni Wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima na baadaye alihamia gazeti la Mwana halisi.Mazishi ya Isango yatafanyika Jumamanne Mkoani Singida.


0 Comments