Mkurugenzi wa Jamii Forum Maxence Melo pichani juu amepata dhamana leo baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili huku kila mmoja alisaini dhamana ya maneno ya Sh.Mil.5 na kuachiwa huru na Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam Godfrey Mwampamba.
Melo alishikiliwa na Polisi zaidi ya saa 72 kabla ya kupandishwa Mahakamani Ijumaa Desemba 16 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na makosa manne likiwemo la kuzuia upelelezi wa polisi.Kesi hiyo itatajwa tena Desemba 29 mwaka huu.
SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA DHARURA NJE YA HOSPITALI KWA
KUSHIRIKIANA NA WADAU BINAFSI
-
NA WAF
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya itaendelea kutekeleza mkakati wake wa
kuimarisha huduma za dharura nje ya hospitali kwa kushirikiana na wadau
bin...
24 minutes ago
0 Comments