MITANDAO YA KIJAMII KUFUNGWA DRC

Umoja  wa Mataifa  umebainisha  wasiwasi  wake  kufuatia  kutangazwa  mpango  wa serikali  ya Jamhuri ya Kudemokrasia ya Kongo  (DRC), kufunga   kufunga  kitandao ya kijamii kuanzia  usiku wa kuamkia leo.

Kamishna Mkuu wa haki za  binadamu  wa UN , Zeid Ra'ad Al Hussein amesema  hatua hiyo  ya DRC, inayoenda  sambamba na  marufuku  ya maandamano  ya mashirika  ya kiraia  na vyama  vya upinzani, imefanyika katika mkesha  wa siku ambayo ni mwisho  wa Rais Joseph Kabila kuwa  madarakani kwa mujibu  wa katiba  ya nchi hiyo.

Ra'ad  alisema  ana wasiwasi  kwa kuwa  serikali ya DRC imetaka  mashirika  yanayotoa huduma  za intaneti  na simu  kufunga mitandao  ya kijamiiJumapili usiku akusema kitendo hicho  kinaongeza  mvutano na wasiwasi mkubwa.

Alitoa wito kwa serikali  kubadili uamuzi  huo na  kuhakikisha  haki  ya watu  kujieleza na kupata taarifa kwa mujibu wa katiba  ya DRC inaheshimiwa.

Kwa mujibu wa makubaliano  yaliyofikiwa  na baadhi  ya vyama vya upinzani ,uchaguzi hautafanyika  hadi Aprili  mwaka 2018, huku Rais Kabila  akipanga  kuendelea  kuwa madarakani baada ya leo , Desemba 19 mwaka 2016.

Mazungumzo yanayoratibiwa  na Kanisa  Katoliki nchini DRC yamekuwa  yakiendelea  Jijini Kinshansa  kujaribu  kutafuta suluhu ya muelekeo wa uongozi baada ya leo ikiwa ni katika kuepusha machafuko nchini humo.

CHANZO CHA HABARI , AFP

Post a Comment

0 Comments