|
Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (katikati mbele), akisindikizwa na wanachama wa
chama hicho, alipowasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju,
wakati CCM ilipozindua kampeni kwaajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika
jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana. PICHA/JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG |
|
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (kulia)
akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba mbele
ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya
Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni kwaajili ya
uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana. |
|
Katibu
Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba
‘Gadafi’ (kulia) akimpongeza Mgombea
Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba baada ya kumkabidhi
Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama
wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko
Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam
jana. |
|
Katibu
Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba
‘Gadafi’ (kushoto) akimtambulisha Mgombea
Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba baada ya kumkadhi
Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa
wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya
Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini
Dar es Salaam jana. |
|
Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (kulia), akiusalimia umati wa wanachama wa chama
hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya
Bunju, baada ya kutambulishwa na kukabidhiwa Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi
Mkuu wa Mwaka 2015, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es
Salaam jana. Kulia kwake ni Katibu Mwenezi wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Juma
Simba ‘Gadafi’. |
|
Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akizungumza umati wa wanachama wa CCM na
wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati
wa uzinduzi wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo
hilo, jijini Dar es Salaam jana. |
|
Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akiinadi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu
wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi
waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa
uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana. |
|
MAMA
MZAA CHEMA … Mama Evelyne Warioba ambaye ni mama mzazi wa Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akiusalimia umati wa wanachama wa chama hicho na
wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati
wa uzinduzi huo. |
|
Sehemu
ya umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na wananchi waliofurika
katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. |
|
Meya mstaafu
wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa akimwaga sera za CCM mbele ya umati wa
wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya
Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. |
|
Mhamasishaji
maarufu kwa jina la ‘Msaga Sumu’ naye alikuwepo. |
MANISPAA ya Kinondoni imetenga fedha kiasi cha Sh. Bil.1 ambazo zitagawiwa
katika kata kumi kwa ajili ya mikopo
isiyokuwa na masharti kwa vijana.
Hayo yalisemwa
na Mtashiki Meya wa Kinondoni Yusuph
Mwenda alipokuwa akimnadi mgombea wa Ubunge Kawe kwa tiketi ya Chama
Cha Mapinduzi Kippi Warioba kwenye viwanja vya Boko CCM Jijini Dar es Salaam.
Aliongeza
kwa kusema kuwa tayari Manispaa imetenga kiasi cha Sh.Bil. 1 kwa jimbo la Kawe
ambapo kila kata itapata Sh. Mil.100
ambazo zitatolewa mikopo bila masharti kwa vijana.
Mwenda
aliongeza kwa kusema kwamba fedha hizo ambazo zimetolewa na CCM ni mwendelezo
kwa kuwawezesha vijana na kwa katika kipindi kilichopita walitoa
mikopo bila masharti kwa vijana yenye
thamani ya Sh.Mil 500.
“Endapo mtachagua wagombea wa CCM itakuwa ni
kazi rahisi kwa serikali yetu
ijayo itakayokuwa chini ya Rais Magufuli
wote kwa pamoja wataweza kukaa na kuzungumza namna ya kumalizia ujenzi
wa Hospitali ya Mabwepande na maendeleo mengine mengi tu yatakuja endapo
mtamchagua Warioba” alisema.
Aliongeza
kwa kusema kuwa licha ya kuwa kwa kipindi kilichopitita CCM haikuwa na Mbunge
wa Kawe lakini serikali kwa kupitia
Manispaa ya Kinondoni imefanikiwa kutatua migogoro mingi ya ardhi ikiwemo wakazi wa eneo la Chasimba ambao hivi
karibuni watapewa haki ya kumiliki ardhi
hiyo kwa kila mmoja kupatiwa hati miliki.
Mwenda
aliongeza kwa kusema kwamba CCM hawatakubali kupoteza nguvu za maendeleo
waliyoyaanzisha huku akiwasisitiza
wakazi wa Kawe waichague CCM kuanzia madiwani , mbunge na rais ambaye ni John
Magufuli.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo Warioba alisema kwamba atazingatia suala zima la migogoro
ya ardhi Kinondoni na kwa wakazi wa
Kawe.
“Nitakaa na
wadau wote wa Kawe kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili
kwani nayajua matatizo yenu yote, nayafahamu matatizo ya Jimbo la Kawe kwa
ujumla” alisema Warioba.
Aliongeza
kwa kusema kwamba atahakikisha anatatua tatizo la ukosefu wa matundu ya vyoo
katika shule za Kawe hivyo atakuwa na vikao vingi katika kila kata kuwasikiliza
na kuweka mikakati ya kurudisha jimbo hilo CCM kwani hivi sasa linashikiliwa na
Halima Mdee Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo( Chadema).
Aidha
Warioba alitumia muda wake kuwaombea kura madiwani kumi wa Kawe ambao wanawania
nafasi hiyo kwa kusema kuwa ili aweze kufanya kazi vizuri anaomba wananchi
wachague madiwani wa CCM, Mbunge CCM na Rais wamchague wa CCM
ambaye ni John Magufuli.
0 Comments