Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete amewasili katika mji mkuu wa Afrika Kusini wa Pretoria
usiku wa leo, Jumatatu, Desemba 9, 2013, kuhudhuria Ibada Kuu ya Kitaifa
(Memorial Service) ya msiba wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson
R. Mandela kwenye Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg.
Rais
Kikwete anajiunga na mamia ya viongozi wa nchi mbali mbali duniani kuomboleza
kifo cha mmoja wa viongozi mashuhuri zaidi duniani katika karne za 20 na 21.
Rais
Kikwete ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa Pili wa Zanzibar, Balozi Seif Ali
Idd na mkewe Mama Asha; Mama Salma Kikwete na Ndugu Abdulahramani Kinana,
Katibu wa Mkuu wa CCM.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa
Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria alikowasili usiku
wa kuamkia leo tayari kuhudhuria mazishi ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee
Nelson R. Mandela.
(PICHA NA IKULU)


0 Comments