Bondia Floyd Mayweather Jr (kushoto)
akimsulubu Robert Guerrero katika pambano la masumbwi kwenye Ukumbi wa
MGM Grand Garden, jijini Las Vegas, Marekani. Mayweather Jr alishinda
kwa pointi pambano hilo la kwanza tangu amalize kifungo cha miezi miwili
jela.
Mayweather Jr akiendelea kumuadabisha
Guerrero, kiasi cha majaji wote watatu kumpa ushindi sawasawa wa pointi
117-111 na kutwaa ubingwa wa Dunia wa WBC uzani wa ‘welter.’
Guerrero akiwa na jeraha juu ya jicho la kushoto lililotokana na makonde mazito ya Mayweather Jr.
Guerrero akipewa maelekezo na kocha
wake, wakati wa mapumziko ya moja ya raundi za pambano hilo, ambalo
alipigwa kwa pointi na kukiri mpinzani wake ni mjanja na ana kasi kubwa
ulingoni.
Mayweather Jr (kushoto), akikwepa fataki la kushoto kutoka kwa Guerrero katika pambano hilo.
Guerrero akiendelea kushambulia 'upepo'
kutokana na Mayweather Jr kuwa mbunifu katika kukwepa makonde yake kama
anavyoonekana pichani.
Mayweather akaweka mzaha kando na
kuanza kujibu mapigo, ambapo makombora yake yalikuwa yakitua sawasawa
mwilini mwa Guerrero, ingawa hayakuweza kumdondosha na kuishia kumuumiza
tu na kutokwa damu.
Guerrero akipokea konde zito la Mayweather. Baada ya pambano, Guerrero alikiri kushindwa na kumsifia mpinzani wake: "Nilimpiga
baadhi ya makonde mazuri. Lakini yeye ni bondia mkubwa na bora. Ni mjanja na mwepesi
mno ulingoni"
Mayweather Jr akiwa amebebwa baada ya
kutangazwa mshindi kwa pointi 177-111 kutoka kwa majaji watatu wa
mtanange huo ndani ya Ukumbi wa MGM Grand Garden, Las Vegas, Marekani.
Mayweather Jr (kulia mwenye kapero)
akishangilia ushindi wake na baba yake Mayweather Sr (kushoto), huku
wapambe wake wakinyanyua juu mikanda anayoishikilia baada ya ushindi
wake dhidi ya Guerrero.
Mayweather baada ya pambano hilo alisema: "Najisikia vibaya kwa sababu sikuweza kushinda kwa ‘knockout’
ambayo mashabiki wangu walikuwa wakitaka. Nilipigana kadri niwezavyo
kuhakikisha nashinda kwa ‘knockout,’ lakini hilo halikutokea ulingoni"
0 Comments