KILI MARATHON KWENYE PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI




Mgeni rasmi katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2013, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akiwahutubia washiriki na wakazi wa mjini wa moshi muda mfupi baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mbizo hizo kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Moshi. (MUCCoBS). (Picha na Dixon Busagaga)


Baadhi ya washiriki wa mbio kujifurahisha ‘Vodacom 5 Km Fun Run,’ wakishiriki katika mbio hizo ambazo ni sehemu ya Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2013. (Na Mpiga Picha Wetu)



Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen, akimaliza mbio za Kilimanjaro Premium Lager Half Marathon, zilizofanyika jana mjini Moshi.



Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza kwa wanawake, Zakia Mrisho katika mbio za Vodacom 5 KM, za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2013, mjini Moshi. (Picha na Dixon Busagaga)




Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, akimpongeza mshindi wa mbio za kilomita 21, Sarah Ramadhani, kwa wanwake, katika mashindano ya Kilimanjaro Premium Lager Marathon, zilizofanyika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.





 
Wakimbiaji wa Kenya wakipongezana baada ya kufanya vizuri katika mbio hizo.
Mfukuza Upepo kutoka Nchini Kenya na Mshindi wa Medali ya Dhahabu katika Mbio za Kilimanjaro Marathon akienda kumaliza mbio hizo hii leo katika Uwanja wa Michezo wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
Eunice Muchiri akikimbia na kumaliza wapili mbio za Kilimeta 42 Wanawake, katika Mbio za Kilimanjaro Marathon akienda kumaliza mbio hizo hii leo katika Uwanja wa Michezo wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
Hakika mbio si kitu lelema, hapa ni Eunice Muchiri akitaapika baada ya kumaliza mbio hizo.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen akimaliza kukimbia Kilometa 21 katika mbio za nyika za Kilimanjaro 2013. Poulsen amedhihirisha kuwa ni mwanamichezo na kuwa kocha wa Kwanza wa Timu ya Taifa kushiriki mbio hizo tangu kuanzishwa kwake miaka 10 iliyopita.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen akisalimia mashabiki waliokuwa wakimshangilia baada ya kumaliza kukimbia Kilometa 21 katika mbio za nyika za Kilimanjaro 2013. (Picha na Father Kidevu Blog)

Post a Comment

0 Comments