Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) na Balozi wa Ambwene
Yessaya 'AY' akiwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kumwezesha
kupata tuzo hiyo kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na
kushoto ni DJ wake Athur Baraka.
**************** Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakiwa na
balozi wake Ambwene Yessaya “AY” leo wamewashukuru watanzania kwa
kumpigia kura msaani maarufu wa kizazi kipya Ambwene Yessaya “ AY “ na
kumwezesha kuibuka mshindi wa tuzo ya kwanza katika kipengele cha Most
Gifted East African video of the Year kupitia kibao chake kipya
kijulikanacho kama “ I don’t wanna be alone”
Akiongea na
wandishi wa habari katika Ofisi za Airtel leo AY amechukua fulsa
kuwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kuweza kumwezesha kuibuka na
ushindi. Aidha alivishukuru vyombo vya habari kwa kuendelea
kushirikiana naye katika kufikisha habari na kumsaidia kupata tuzo hiyo.
Naye
Afisa uhusino wa Airtel Jane Matinde alisema” tunafurahi kuona msanii
AY ambaye ni balozi wetu kuibuka na tuzo iliyoshirikisha wasanii
mbalimbali toka Afrika, sisi tunasikia furaha kuona mafanikio ya
wasanii wetu nchini yakiendelea kukua na ndio sababu leo tuko hapa
kusherehekea ushindi huu kwa pamoja na kuwashukuru watanzania kwa
kumuwezesha AY kupata tuzo hii kwa kura zenu.
Tunapenda pia
kuchukua fulsa hii kuwaalika watanzani na wateja wetu leo pale nyumbani
lounge usiku kuanzi saa tatu tuweze kujumuika na AY na kumpongeza kupata
tuzo hii. Tutakuwa na wasanii wengi pamoja na wadau mbalimbali wa
Musiki na pia utapata muda kupiga picha na msanii huyo na Tuzo yake
|
0 Comments