Social Icons

Friday, June 10, 2016

KANISA LA SINZA CHRISTIAN CENTRE LATUPIWA VYOMBO NJE

Kutokana na kudaiwa deni la zaidi ya mil 100 kanisa la Sinza Christian Center  latupiwa  nje vyombo vyake na dalali aliyepewa tenda hiyo bwana Joshua aliyeteuliwa na Mahakama na mmiliki jengo hilo Bwana Prosper Rwendera , akizungumza na Dar es salaam yetu Blog  mke wa mmiliki  wa jengo Hilo Bi. Patricia Prosper Alisema; “huyu aliyepanga hapa hakufuata utaratibu wowote na ndiyo maana tukapewa jengo letu." 

Alipotafutwa msemaji wa Kanisa ambaye ni Askofu anayedaiwa kuvamia jengo hilo, hakupatikana kuzungumzia sakata hilo na hata waumini wa kanisa hilo walipotafutwa walikataa kwa madai hawana mamlaka ya kuzungumzia lolote kuhusiana na sakata hilo.

Hili ni eneo la Kanisa Hilo
Viti  vyote vikiwa vimetolewa nje
 Vyombo vya Muziki vikiwa nje
 Magari yakiwa yanatolewa nje
 Vitu vikiwa nje ya Jengo hilo ambapo mpaka sasa kuna sinto fahamu vinapelekwa wapi
 Vikombe nje
 Wametoa vitu vyote
Magodoro na vitanda vyote nje  
 Baadhi ya Magari yaliyotolewa katika Jengo hilo ambapo hapo awali ilikuwa ni Kanisa
Kushoto kwa mbali ni Mke wa Miiliki wa Jengo hilo Bi. Patricia Prosper akiendelea na majukumu huku pembeni vijana wakipata maelekezo ya kuendelea kutoa vitu.
 Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa
Regards Tone Multimedia Company Limited Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 E-Mail blogszamikoa@live.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa Web: www.blogszamikoa.com

No comments:

 
 
Blogger Templates