Social Icons

Thursday, June 9, 2016

WANAHARAKATI WATOA TAMKO LA PAMOJA KUHUSU BAJETI YA TAIFA ILIYOSOMWA JANA BUNGENI DODOMA


TGNP Mtandao kwa kushirikiana na wanaharakati ngazi ya jamii kutoka maeneo mbali mbali ya Dar es Salaam, Mbeya, Morogoro, Shinyanga, na washiriki wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS), Kikundi Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BATT) na Asasi nyingine za Kiraia wamefanya maandamano wakiwa wameshika mambango yenye ujumbe pamoja na kutoa tamko baada ya kufanya uchambuzi wa kina na kuainisha maboresho na mapungufu ya bajeti ya Taifa ya mwaka wa fedha 2016/17 iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (MB) tarehe 08 Juni 2016 Bungeni Dodoma.Picha na Geofrey Adroph.
Wanaharakati kutoka Ngazi ya jamii na wanachama wa vituo vya taarifa na maarifa wakiwa kwenye maandamano
 Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi Lilian Liundi(KUshoto) akiwa amebeba moja ya bango pamoja na Mwanaharakati kutoka Ngazi ya jamii ili kuonesha umma masuala yaliyosaulika katika bajeti hiyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake katika Jitihada za Maendeleo (WAJIKI), Janeth Mawinza akitoa tamko bajeti ya Taifa iliyo somwa Jana Bungeni mbele ya wandishi wa habari (hawapo pichani) leo katika ofisi za TGNP Mtandao.
Mwanaharakati Nyanjura Kalindo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) akitole msisitizo kuhusu tamko lao lililotolewa kuhusu Bajeti ya Taifa iliyosomwa Jana Bungeni.
Mwandishi wa Channel Ten akiuliza swali kwa Wanaharakati kutoka Ngazi ya jamii na wanachama wa vituo vya taarifa na maarifa mara baada ya kutoa tamko kuhusu Badger ya Taifa iliyo somwa Jana Bungeni.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi Lilian Liundi akitolea ufafanuzi moja ya swali lililoulizwa na mwandishi wa habari.
Mwanaharakati kutoka Kigamboni, Bi. Subira Abdalah Kibiga akitolea ufafanuzi moja ya moja ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari wakati wanatoa tamko lao mbele ya waandishi wa habari kuhusu Bajeti ya Taifa iliyosomwa jana Bungeni mjini Dodoma.
Mwanaharakati Selemani Bishegezi akijibu akijibu swali lililoulizwa na mmoja wa waandishi wa habari
Baadhi ya Wanaharakati kutoka Ngazi ya jamii na wanachama wa vituo vya taarifa na maarifa wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu Bajeti ya Taifa iliyo somwa Jana Bungeni.

No comments:

 
 
Blogger Templates