Social Icons

Saturday, July 4, 2015

SIMBA YAZINDUA HUMA MPYA YA 'SIMBA NEWS' KUPITIA MTANDAO WA TIGO















Mkurugenzi wa EAGGroup Imani Kajula  (Kushoto) akifafanua jambo katika mkutano huo jana akifuatiwa na   Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, akifuatiwa na Meneja Mawasiliano  ya Kibiashara  wa Tigo  Jacqueline Nnunduma wakati walipozungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam  wakati wa uzinduzi wa huduma ya Simba News kupitia Simu za mkononi za Tigo, ambapo mteja atajiunga kwa kuandika neno SIMBA kwenda namba 15460, kisha kukatwa sh. 150 kwa siku.
KWA mara nyingine tena Klabu ya  Simba  wamezindu huduma ya kuwapasha habari mashabiki wake kwa kupitia simu za mkononi itakayofahamika kwa jina la ‘Simba News’.
Akizungumza jana katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam Rais wa klabu hiyo Evance Aveva alisema kwamba Simba watashirikiana na Kampuni ta Tigo katika kuhakikisha  mashabiki wake wanapata taarifa za timu yao.
“Huu ni mwanzo hivyo mashabiki wakae mkao mzuri kwani mambo mengi mazuri yanakuja kwa sababu tuko katika hatua za mwisho na Kampuni zingine za simu ambao nao watakuwa wakitoa huduma kama hii ili kuweza kuwafikia mashabiki wetu kwenye mitandao yote” alisema Aveva.
Aveva aliongeza kusema  anampongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya EAGGroup Imani Kajula ambao ni wasimamizi wakuu wa tovuti ya klabu hiyo  pia wamekuwa ni washirika wao katika upande wa kibiashara kwa kuweza kuwa wabunifu katika  kuiwezesha Simba ikijingaza kitaifa na Kimataifa pia uwepo wao ndani ya Simba kumeleta tija.

Mkurugenzi wa EAGGroup Imani Kajula aliongeza kwa kusema kuwa wao wanatambua umuhimu wa kutoa taarifa hivyo wameanza na Tigo kwa huduma ya Simba Sms ambayo itagharimu kiasi cha sh. 150 tu huku akitoa wito kwa mashabiki kujiunga na huduma hiyo ili waweze kupata taarifa za timu yao.Ili kujiunga shabiki atatakiwa kuandika neno SIMBA  kwenda 15460. 

No comments:

 
 
Blogger Templates