Social Icons

Friday, April 24, 2015

ALLY CHOKI KUTUPA KARATA YAKE YA 13 TWANGA PEPETA


MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki wa dansi nchini Ally Choki Aprili 25 mwaka huu atapanda katika jukwaa la bendi ya Twanga Pepeta na kuimba wimbo wake wa 13.
Choki alirudi kundini mapema mwezi uliopita atazindua wimbo wake wa 13 ndani ya bendi hiyo unaokwenda kwa jina la 'Kichwa Chini'.

Kumbukumbu zinaonesha kwamba kabla ya kuondoka katika bendi hiyo ya Twanga aliacha nyimbo zake 12 ambazo zote zilikuwa moto wa kuotea mbali.
Nyimbo 11 za Choki ambazo aliwahi kuziimba ni pamoja na ‘Busu la 2001’,  ‘Mtaa wa Kwanza’, ‘Walimwengu’, ‘Password’ ,’All Eyes on me’, ‘Uvumilivu, Furaha ya Harusi, Jirani , ‘Chuki  Binafsi’, ‘Binadamu Roho ya Kwanini’ na  ‘Umbea Hauna Posho’.
Wimbo ambao choki atautambulisha leo ambao ndiyo atakaokata utepe akiwa jukwaani unakwenda kwa jina la ‘Uso Chini’ tayari umesharekodiwa na kusambazwa katika vituo mbalimbali vya redio na luninga nchini.

Akizungumza jana Mkurugenzi Mtendaji wa bendi hiyo Asha Baraka alisema kwamba onyesho hilo la utambulisho litakuwa la  aina yake hivyo siyo la kukosa .

Akizungumzia kwa upande wa  mtindo gani ambao Choki ataingia nao ukumbini kama jinsi ambayo amekuwa akifanya huko nyuma katika maonyesho mbalimbali alisema mwanamuziki huyo ni mwenye ubunifu wa hali ya juu hivyo kila shabiki ajitokeze ukumbini kesho mapema ili awahi nafasi yake na kuona kile ambacho Choki amewaandalia mashabiki wake.
“Siwezi kusema Choki ataingia kwa mtindo gani ukumbini kwani hiyo bado ni siri yake, pia mnenguaji Mussa Hassan ‘Super Nyamwela na mpiga kinanda mahiri Victor Mkambi wote watatambulishwa rasmi” alisema Asha.

Asha alisisitiza kwa kusema kwamba mandhari ya ukumbi wa Mango Garden itabadilika kutakuwa na jukwaa jipya na viti vipya hivyo kila kitu kwa siku ya  Jumamosi.
Kiingilio cha onyesho hilo siti maalum ni sh.15,000 na kawaida 10,000.

No comments:

 
 
Blogger Templates