Social Icons

Thursday, February 19, 2015

MWAKILISHI JIMBO LA MAGOMENI ZANZIBAR AFARIKI GHAFLA AKIWA KIKAONI CCM KISIWANDUZI

MWAKILISHI wa jimbo  la Magomeni ambaye pia ni Mnadhimu  Mkuu wa Baraza  Salmin Awadh Salmim pichani juu  amefariki dunia ghafla jana  mchana wakati alipokuwa akishiriki  katika kikao  kilichokuwa kikifanyika katika Ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Kisiwandui, Zanzibar.

Kwa mujibu  wa taarifa  iliyotolewa na Katibu wa Baraza  hilo Yahya Hamis Hamad alithibitisha taarifa za kifo hicho na kusema maandalizi ya mazishi yameanza na marehemu ataagwa kesho saa5  na maziko yatafanyika  kesho Ijumaa Makunduchi nje ya mji wa Zanzibar.

Ilielezwa kwamba marehemu alifikwa na mauti ghafla wakati alipokuwa akishiriki kwenye kikao cha sekretarieti ya CCM.

Marehemu alikuwa alikua Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM  Zanzibar .
Aidha marehemu hakuwahi kuwa na taarifa za ugonjwa wa aina yoyote au kulalamika kusumbuliwa na ugonjwa wowote katika enzi za uhai wake.
Bali  mwezi mmoja uliopita alikwenda nchini India ambako hakuna anayejua kama alikwenda kutibiwa au alikwenda kuangalia afya yake.
Kwa wiki tatu zilizopita alikwenda nchini Korea mbako alikwenda kushiriki kuzinduliwa kwa meli mpya ya Zanzibar ambako alishiriki kuiweka katika maji na alirudi nyumbani akiwa mwenye afya.

No comments:

 
 
Blogger Templates