Social Icons

Thursday, February 19, 2015

TWANGA & FM ACADEMIA KUTUMBUIZA PAMOJA MACHI 28 LEADERS CLUB

WADAU wa muziki wa dansi watapata burudani ya aina yake  katika onyesho maalum ambalo litawakutanisha pamoja  bendi  kongwe za muziki  wa dansi za Twanga Pepeta na FM Academia.
Onyesho hilo ambalo limepangwa kufanyika  Machi 28, kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Itafahamika kwamba bendi hizi mbili ambazo kuna wakati walikuwa mahasimu  wakuu hali iliyopelekea kuwa na upinzani wa hali ya juu.
Aidha wadau wamezibatiza jina na kuwaita Ukawa wa kudumu ambapo watapanda jukwaani kwa mara ya kwanza  na kutumbuiza pamoja.
 Hii ni kwa sababu hizi ni bendi pekee za kizazi cha tatu cha muziki wa dansi nchini ambazo zimedumu muda mrefu na zina washabiki wengi zaidi.

 Hii ni sawa sawa na Msondo na Sikinde  (bendi za kizazi cha pili cha muziki wa dansi nchini) walivyoanza mipambano  mwaka 1991.  Hivi sasa imekuwa kama Simba na Yanga kwa vile mpira ni tofauti na muziki, ilikuwa ni muhimu kuwa na aina nyingine ya mpambano wa kizazi kipya.
 Akizungumza na Jana Meneja wa bendi ya Twanga Pepeta Hassan Rehan alisema  pambano hili  ni moja ya njia ya kurudisha umaarufu wa muziki wa dansi nchini.
Muziki wa Bongo Fleva una chachu kubwa ya tamasha la Fiesta ambayo hukutanisha wanamuziki wengi pamoja  hivyo muziki wa dansi ulikuwa hauna matukio ya kuzikutanisha  bendi tofauti kiushindani ukiachia kwenye kusindikiza uzinduzi wa album mpekee.
Kwa upande wa FM Academia watakaopanda jukwaani ikiwa na ‘Dream Team’ kundi linaloundwa  na   Rais wa bendi hiyo Nyoshi El Saadat , Patcho Mwamba, King Blaise, Pablo Masai, Levi Boy, Totoo Kalala, Kalidjo, G-seven, Elombe Kisinja,  Moses Ebonga Katumbi ‘Jesus’ ,Baratele Hatibu na wengine wengi .
Huku bendi ya Twanga Pepeta ikiongozwa na Kiongozi wa bendi Luizer Mbutu, Haji  Ramadhani,  Kalala Junior, Saleh Kupaza na wengine.

No comments:

 
 
Blogger Templates