Social Icons

Friday, February 27, 2015

BLOGGERS WA TANZANIA NA NJE (DIASPORA) KUANDIKA HISTORIA FEB:28 SERENA HOTEL

  Father Kidevu (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano
Baadhi ya Bloggers na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari Maelezo Dar es Salaam leo mchana.
 Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano huo ambapo pia alitoa wito kwa wanaandishi wa habari wa kike kujitokeza kwa wingi katika kuanzisha blogs zao na kujikita kwenye amasuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kupiga vita ukatili  wa kijinsia, unyanyapaa kwa wenye ulemavu wa ngozi na mauaji ya Albino.
   Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano.
Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network  na mmiliki wa Blog ya The Habari.com Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi. Kutoka kushoto ni  Mkala Fundikira,Shafiq Mpanja wa AM,Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale na Khadija Kalili .Sherehe hiyo ya Bloggers inatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Serena  Hotel ambapo  mgeni rasmi atakuwa Katibu wa  Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga ambapo pia viongozi kutia Jukwaa la Wahriri Tanzania na watu wengine mashuhuri wamealikwa. Sherehe hiyo imedhaminiwa na Kampuniu ya simu ya Vodacom, NMB na Kampuni ya AM.
 (Picha Zote na Mroki Mroki).

No comments:

 
 
Blogger Templates