Social Icons

Friday, November 28, 2014

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KUZINDUA ALBAMU YA USILIE DES.7 PTA

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa kwaya ya  Family Singers Jonas Danny akifafanua jambo katika mkutano na wandishi wa habari hawapo pichani wakati wakizungumza nao katika mkutano kuhusu uzinduzi wa DVD  ya usilie itakayozinduliwa Desemba 7 mwaka huu katika ukumbi wa PTA Dar es Salaam anayefuata ni Daniel Misheto kutoka Misheto Promotion.

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ametajwa kuwa mgeni rasmi kwenye  uzinduzi wa  albamu  ‘Usilie’ ambayo itapatikana kwenye DVD Desemba 7 mwaka huu.
Akizungumza jana kwenye mkutano na waandishi wa habari Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’  Danny Misheto alisema kwamba hafla hiyo itafanyika kwenye uwanja wa Sabasaba ulioko barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Mbali ya uzinduzi huo pia wasanii mbalimbali wa filamu watanogesha siku hiyo.

Aidha waimbaji wa injili ambao ni Leah Mudy ,AIC (T) Vijana Chang’ombe, Accasia Singers, Papson Mastaki kutoka Kenya na Frank Hume kutoka Boston nchini Marekani watatumbuiza.
Uzinduzi huu umeratibiwa na Misheto Promotion  ambapo kabla ya uzinduzi huo kutafanyika  huduma za bure za kiafya na kitabibu kutoka kwa madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali ambayo yamekuwa yakiikabili jamii.

Misheto anayataja magonjwa hayo kuwa ni moyo, figo, kisukari  na mengineyo ambapo huduma hiyo itatolewa na madaktari bingwa nchini.

“Huduma hii itaanza saa mbili asubuhi  na itatolewa bure , ikiwemo ushauri na kwa wale ambao wataweza kutibika watatibiwa ila ambao watakuwa kesi zao zimekuwa ni kubwa zaidi watapewa ushauri wa bure wa kuendelea na matibabu katika hospitali kubwa” na kiingilio ni bure alisema Misheto.

No comments:

 
 
Blogger Templates