ARUSHA, Tanzania
KATIKA kuhakikisha Watanzania wanakuwa na afya bora, kinywaji kisicho na kilevi cha Vita Malt, kimeandaa bonanza maalumu litakalowashirikisha wafanya mazoezi ambalo linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya General Tyre, jijini hapa leo.
KATIKA kuhakikisha Watanzania wanakuwa na afya bora, kinywaji kisicho na kilevi cha Vita Malt, kimeandaa bonanza maalumu litakalowashirikisha wafanya mazoezi ambalo linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya General Tyre, jijini hapa leo.
Meneja
wa Vinywaji visivyo na Vileo katika Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
Consolata Adam alisema, baada ya kufanyika Dar es Salaam na Mwanza
wameamua kulileta Arusha kabla ya kuelekea Mbeya.
Kuhusu
bonanza la leo, Consolata alisema, anaamini litakuwa la aina yake na
linatarajiwa kuanza saa 2 asubuhi na kuwataka wakazi wa Arusha kufika
kwa wingi uwanjani hapo ili kufanya mazoezi kwa pamoja.
“Tumeamua
kuandaa bonanza linalowakutanisha wanamichezo mbalimbali hasa wafanya
mazoezi ili kuweza kukutana na kufanya mazoezi kwa pamoja.
“Katika
bonanza hilo kutakuwa na gym maarufu za Arusha ambazo zitashiriki na
kutakuwa na wakufunzi mbalimbali,” alisema, huku akidai mtu anatakiwa
kwenda tu uwanjani kwani mazoezi hayo yatakuwa bure.
Alisema,
lengo kuu kuu la bonanza ni kuhamasisha jamii nzima kutambua umuhimu
wa kufanya mazoezi ili kujenga afya bora za miili yao na pia kujenga
umoja imara wa gym zilizopo nchini.
Burudani katika bonanza hilo inatarajiwa kutolewa na bendi ya Vita, huku wasanii maarufu wa Bongo Fleva wa Arusha nao wakiwepo.
“Tumeweka
burudani za kila aina kwani kutakuwa na michezo mbalimbali ya
kufurahisha kama soka, netiboli, kuvuta kamba, kukimbiza kuku pia na
zawadi nyingi toka Vita Malt zitakuwepo.”
Naye
Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa TBL, Edith Mushi aliwataka wakazi wa
Arusha kutumia fursa hii hili kufanya mazoezi kwa pamoja.
“Hii ni siku ya familia napenda kuwajulisha watanzania wote na wapenda michezo kote nchini kuwa waje mapema na familia zao.”
Vita Malt ni kinywaji kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
0 Comments