Social Icons

Wednesday, July 25, 2012

MAKALLA STUDIO ILIYOTOLEWA NA RAIS BADO HAIJAZAA MATUNDA KWA WASANII

Naibu Waziri Wizara ya  Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Amos Makalla.


NAIBU Waziri  wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Maklla amesema kuwa studio ya muziki iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuwanufaisha wasanii wa ndani bado haijazaa matunda kwa wasanii hao.

Alisema pamoja na nia njema ya kutaka kuwasaidia wasanii lakini wajanja wachache wamekuwa wakijinufaisha wao wenyewe kwa kutafuna fedha za studio hiyo.

Alisema wasimamizi wa studio hao wamethubutu kutafuna kiasi cha sh. Milioni 9.6 zilizotolewa na Rais Kikwete kwa ajili ya pango la studio hiyo na bila aibu wamekuwa wakiomba fedha nyingine kwa ajili ya pango.

Hata hivyo Makalla alisema kuwa kutokana na studio hiyo kutokuwa na tija serikali kwa sasa inafanya utaratibu wa kurudisha studio hiyo serikalini  na iwe chini ya usimamizi wa BASATA.

Aidha alitangaza kiama kwa baadhi ya wajanja ambao wanafanya ujanja wa kuiba kazi za wasanii kwa kudurufu kazi zao kwa lengo la kujinufaisha  wenyewe badala ya wasanii kunufaika.

Alisema kutokana na hali hiyo ni bora wale wote wenye mitambo ya kudurufu kazi za wasanii ambao wana tabia ya kuwaibia wasanii wazirejeshe wenyewe la sivyo watachukuliwa hatua kali.

Akiendelea kuelezea kuelezea hoja ya Upinzani bungeni, Makalla alisema kuwa juhudi za mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Chadema), ambaye pia ni Waziri kivuli wa Wizara hiyo ni msaada mkubwa kwa serikali na wasanii kwa ujumla. 

No comments:

 
 
Blogger Templates