Social Icons

Friday, February 3, 2012

ROSE NDAUKA AJA NA REAL PROMISE

Kampuni ya Faisal Production ikiwa miongoni mwa taasisi chache zenye lengo maalum la kuhakikisha fani ya filamu inastawi na kupata maendeleo nchini, imeandaa muvi mpya inayokwenda kwa jina la REAL PROMISE ambayo inatarajiwa kuwa madukani mwezi Februari.

Katika filamu hiyo ambayo tayari imeanza kuwa gumzo la jiji, waigizaji nyota kama Mohammed Mwikongi ‘Frank’, Rose Ndauka, Bambucha na Rania wameshiriki na kufanya makubwa ambayo yatamfanya mtazamaji kutopata muda wa kufanya shughuli nyingine.

Kwa mujibu wa msemaji wa kampuni hiyo, Feisal, filamu hiyo kwa sasa iko hatua ya uhariri huku mtunzi wake Pazi akisisitiza kutoa tungo bora kabisa sambamba na Muongozaji aliyepevuka kwa kazi hiyo aitwaye Lee.

Real Promise inazungumzia mikasa ya mapenzi na hatua mbalimbali za kukabiliana nayo ikizingatiwa kuwa mapenzi ni sehemu kubwa ya maisha ya kila siku ya binadamu.

No comments:

 
 
Blogger Templates