Social Icons

Friday, February 3, 2012

NGOME YA LUMOLE NI SHULE TOSHA

Dj Choka.
Nguli wa filamu za Kitanzania, Lumole Matovolwa maarufu kama Biggie, amesema kuwa, mpenzi yeyote wa filamu atakayebahatika kupata nakala ya filamu mpya ya NGOME YA LUMOLE na kuiangalia, atakuwa amepata zawadi ya mafunzo ya bure katika maisha.

Biggie aliyewahi kutamba sana na maigizo ya runinga na baadhi ya filamu nchini, ameliambia gazeti hili kuwa ndani ya filamu hiyo kuna kila aina ya mafunzo toka mitaani, majumbani, maofisini nk ambapo hata upande wa imani kuna mguso wa aina yake unaoonesha yaliyojificha.
\
Aidha, Biggie ameisifu kampuni ya Kiumbe Productions chini ya Meneja wake Hussein Makatta kuwa imepiga hatua kubwa kwa uandaaji na utengezaji wa filamu unaozingatia viwango vya ubora wa kila kitu huku maudhui na mtiririko wake ukithibitishwa kwa vitendo na muda.
Wasanii wengine walioshiriki Ngome ya Lumole itakayoingia wakati wowote kuanzia sasa ni pamwe na Mayasa Mrisho 'Maya', DJ Choka, Mack Star aliyeng'ara na filamu ya Ikwizu na wengine wapya kadhaa ambao uwezo wao kikazi umejidhihiri ndanimwe.
Lumole Matovolwa 'Biggie'.

No comments:

 
 
Blogger Templates