Social Icons

Wednesday, March 30, 2011

MASHUJAA KUTAMBULISHA WAPYA MAKUMBUSHO APRILI MOSI

Bendi ya ziki wa dansi Mashujaa Musica inatarajia kutambulisha rasmi uongozi mpya wakiwemo wanamuziki na wanenguaji wake wapya siku April 1 mwaka huu Jijini Dar es salaam. Hayo yalibainishwa leo na Meneja wa bendi hiyo Mujibu Hamisi alipokuwa akizungumza na waandishi habari kuhusu uongozi huo mpya, wachezaji pamoja na wanenguaji wapya ambao utaijenga Mashujaa mpya kwa kufanya mabadiliko makubwa ya kimuziki. Alisema utambulisho huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho ambao utawaweka wazi mashabiki juu ya Meneja huyo mpya, wanamuziki watano na wanenguaji sita wakiwemo wakike wanne na kwamba hiyo itakuwa chachu ya kufanya vitu vya kushangaza tasnia ya muaizki wa dansi. Mujibu alisema jitihada hizo na madhumuni makuu ya bendi hiyo ni kwa ajili ya kutoa burudani itakayo wapelekea mashabiki wazidi kuhamasika na kujenga ukaribu zaidi kwa mashabiki na bendi hiyo. Katika kunogesha onyesho hilo wamewaalika bendi ya Mapacha Watatu, kutumbuiza siku hiyo. Meneja huyo ambaye awali alikuwa akiwajibika katika bendi ya FM Academia alisema katika wanamuziki wapya mmoja wao atakuwa Rapa kutoka Diamond musika Sauti ya Radi ambaye anatarajia kufanya vitu vipya katika kuboresha zaidi bendi hiyo. Mujibu alisema kwa sasa wanaandaa albam mpya ambayo iko jikoni ila hadi kufikia Juni itakuwa imekamilika hivyo ametuma salamu kwa wapenzi wa bendi wakae tayari kuipokea albam hiyo. Hata hivyo Mkurugenzi wa bendi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mashijaa Investment Mamaa Sakina alisema changamoto katika muziki ni nyingi ila anajitahiji mashabiki wafurahi kutokana na kile kinachotolewa katika bendi yake na endapo kuna kitu chochote ambacho mashabiki wake wanakihitaji katika burudani wasisite kutoa mawazo yao.

No comments:

 
 
Blogger Templates