Social Icons

Thursday, December 30, 2010

LADY JAYDEE AZINDUA MAJI, KUANZIA MWAKANI SHOO MOJA TU

Msanii Nyota nchini LadyJaydee akionyesha maji yenye nembo jina lake.
**********************************************************

Msanii mahiri wa bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee amesema kuanzia mwakani atakuwa akifanya onyesho moja tu kwa wiki ili kujipa nafasi ya kufanya mambo mengine ya kijamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Jaydee ambaye pia ni Balozi wa Fistula hapa nchini alisema pamoja na kujikita katika shughuli hizo pia atakuwa akisimamia biashara zake nyingine mbali na muziki.
Alisema pamoja na kupumzika huko lakini bendi yake ya Machozi itakuwa ikifanya maonyesho yake kama kawaida huku yeye akishiriki nayo siku ya Ijumaa tu katika ukumbi wa Mzalendo Pub.
Jd aliongeza kuwa amepanua wigo katika sekta ya ujasiriamali kwa kufungua mgahawa wenye hadhi ya kimataifa, pia kuanza kuuza maji ya kunywa yenye jina lake.
“Pamoja na kuanzisha mgahawa huo utakaokuwa maeneo ya Namanga, pia ule mgahawa wa Binti Machozi utaendelea kuwepo, na haya maji yanayokwenda kwa jina Lady Jaydee Pure Drinking Water yanatauzwa kwa bei za kawaida”, Alisema.
Aidha, Jd alisema mwakani pia anatarajia kutoa albamu yake yake mpya binafsi ambayo itakuwa ya tano tangu alipoanza muziki.

No comments:

 
 
Blogger Templates