Social Icons

Friday, October 15, 2010

SERIKALI YAMPA TANO CHIPUNGAHELO

Serikali imeyapongeza mashindano na waandaaji wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania kuwa ni Shindano pekee ambalo tangu kuanzishwa kwake limekuwa likifanya vizuri kimataifa
Pongezi hizo za serikali zilitolewa ,kupitia kikao cha pamoja kutathimini mashindano hayo tangu kuanzishwa kwake.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na uongozi wa juu wa Miss Utalii Tanzania walitathimini ushiriki wa miss utalii katika mashindano mbalimbali.
Tangu warembo wa miss utalii walipoanza kushiriki mwaka 2005 wamewahi kupata mataji ya ,Miss Tourism World 2005 –Africa, Miss Africa 2005 -1ST Runner Up, Miss Tourism World 2006 –SADIC, Miss Tourism Model Of The World2006 –Personality, Miss Tourism World 2007 –Africa Bikini na Miss Tourism World 2008 – Internet.

No comments:

 
 
Blogger Templates