Social Icons

Friday, October 22, 2010

MWISHO MWAMPAMBA ALIVYOLONGA NA WANAHABARI

Mwisho Mwampamba kabla ya mkutano na waandishi wa habari .Kwa wale ambao hawajapata fursa ya kukaa naye jamaa huyu ni bonge la msela na alituthibitishia pale alipopewa T-Shirt ikiwa mpya na mikono saafi lakini yeye alikuwa akilalamika haweze kuvaa eti mikono ilikuwa inamboa ,ghala akatoweka akaingia zake maliwatoni na mara aliporudi T-shirt ile haikuwa na mikono tena aliikata tena huku akisema sasa saafi najisikia huru na wakati huohuo Meneja Masoko Furaha Samalu alisikika akisema Mwisho kaharibu fulana yangu. Mwisho akitoa mkono wa shukrani kwa Meneja Masoko Furaha anayeshudia ni Ofisa Uhusiano Barbara.
Meneja Masoko wa Multichoice, Tanzania Furaha akimkabidhi king'amuzi cha kisasa aina ya HD PVR , huku akisema Mwisho atakitumia mpaka liamba aliyesimama katikati ni Meneja Uhusiano wa Multichoice Barbara Kambogi.
Mwisho akipozi kwa picha baada ya kuifanyia ubunifu T-shirt yake.
Mwisho na Mwani Nyangasa ambaye ni mwandishi wa The African wote walisema wamecheza wote utotoni.
Mimi na Mwisho baada ya mkutano.
Mhariri wa Gazeti la michezo la Championi Salehe Ally anayejiita Chipukizi wa Championi naye alikuwepo.
Asha Bani na Mtoto wake Sanda (Sofia) Said wote walikwenda kumlaki Mwisho.
Mwisho akipozi kwa picha na Ofisa Masoko wa Multichoice Furaha Samalu. Hapa akiwa nje ya ukumbi ya kuanza mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam .
Kutoka Kushoto ni Furaha Samalu, Mwisho na Ofisa Uhusiano wa Multichoice nchini Barbara Kambogi.
Mwisho akisikiliza maswali kwa makini.
Aliyekuwa mshiriki katika shindano la Big Brother All Stars Mwisho Mwampamba amesema yupo tayari kushiriki tena endapo ataitwa na katika shindano hilo kwa mara nyingine.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Holiday Inn Jijini Dar es Salaam , Mwisho amekiri kuwa hana kinyongo na ushindi wa aliyekuwa rafiki na mshindani wake katika jumba Uti kutoka nchini Nigeria.

“Sina kinyongo na ushindi wa Uti kwani sisi kundi letu wote tumeibuka washindi isipokuwa Munyaradzi aliyekuwa akiwakilisha nchi ya Zimbabwe kwa kufika hatua ya fainali lakini fedha zilikuwa lazima apate mtu mmoja tu” anasema.

Aliongeza kwa kubainisha kwamba yeye na mshindi huyo ni marafiki na wamekuwa wakiwasiliana hata kabla ya mkutano huo kuanza huku akiwa amepokea zawadi kama Kamera pamoja na Laptop kutoka kwa Uti.

Akizungumzia vitu alivyovikosa wakati akiwa katika jumba lile alisema ni Kamusi ya lugha ya Kiswahili, vitabu ambavyo vinaonyesha ramani ya Tanzania na vivutio vyake ambavyo vingemsaidia kuwathibitishia wenzake kwamba Mlima wa Kilimanjaro uko Tanzania kwani hadi hivi sasa wapo ambao wanaamini kuwa mlina huo uko nchini Kenya.

Kutokana na kuwa yeye amejikita zaidi katika masuala ya Utalii akiwa anaishi Mkoani Morogoro Mwisho ameiomba Serikali kujitangaza zaidi kiutalii, madini na vivutio mbalimbali ambavyo viko nchini huku akisema ni jambo la kusikitisha kuona madini ya Tanzanite yanapatikana Afrika ambapo ni nchi ya Tanzania pekee ndipo yanapochimbwa lakini Bodi yake iko nchini Afrika Kusini.

“Hatujinadi kiutalii, nawashauri Bodi ya Utalii pamoja na Wizara ya Maliasili waunganishe nguvu wajitangaze katika vyombo vikubwa vya habari kama CNN nina hakika serikali ikiamua itaweza kwani siku zote biashara ni matangazo” alisema.

Wakati huohuo Mwisho amesema pamoja na kwamba hakuweza kuibuka mshindi katika shindano hilo anachojivunia ni kupata uzoefu ambao utamsaidia katika maisha yake ya kila siku.
Akielezea kuhusu maandalizi ya harusi yake na mchumba wake Merly ambaye tayari amevisha pete ya uchumba wakati wakiwa ndani ya jumba amesema yanakwenda vizuri pia nilipomuuliza swali endapo mchumba huyo atataka wakaishi nchini Namibia mara baada ya kufunga pingu za maisha Mwisho amesema hilo siyo tatizo kwani yeye ni sawa na kiraka hivyo anaweza kuishimahali popote.

No comments:

 
 
Blogger Templates