Social Icons

Friday, October 22, 2010

MAMBO YA ISHA NA TEVEZ HAYA HAPA

Tevez kushoto ambaye ni mume wa Isha Ramadhani a.k.a Mashauzi katika picha ya pamoja.


NaAbdallah Mensah.

Tukio la aina yake lilitokea hivi karibuni pale mwimbaji wa Jahazi Modern Taarab, Isha Mashauzi alipovunjavunja kwa chuma kizito vioo vya gari la mumewe, Jumanne Tevez, kabla naye hajalipiziwa kwa kufanyiwa kama hivyo na mumewe huyo.

Tukio hilo lilitokea nyumbani kwa Tevez, Tandale kwa Tumbo jijini Dar es Salaam, ambako Isha aliyemuhama mumewe na kuishi kivyake hivi sasa alifika kumtaka Tevez ampe talaka yake kwa lazima kwa madai ya kuwa, amemchoka na hana mpango naye.

Kilichofuata baada ya Isha kufika hapo na kuanza kudai talaka kwa vurugu ni Tevez kumwambia kwa upole kuwa, hasiti kumpa hicho anachotaka bali anatakiwa kufuata taratibu na sheria za kidini wakiwa ni watu waliooana kwa mujibu wa imani ya Kiislamu.

“Nitatoa hiyo talaka unayoidai kwa sababu hata mimi mwenyewe nishagundua kuwa, hapa hakuna tena mapenzi, ila kabla sijakupa ni lazima ufuate taratibu kwa sababu sisi hatukuwa tunakaa kihuni,” alisikika akisema Tevez kumwambia Isha.

Kauli hiyo ilionekana kumkera Isha anayetamba hivi sasa na albamu yake binafsi ya ‘Mama Nipe Radhi’, aliyekurupuka kwa jazba na hasira ambako alichukua aina ya chuma kizito na kwenda kuvunja vioo katika gari la Tevez na kulifanya liwe kama lililopatwa na ajali.

Baada ya Isha kuliharibu vioo vya gari la mumewe huyo, naye Tevez alinyakua gongo zito na kwenda kuvunja vioo vya gari la Isha, ambako katika hekaheka hiyo, Isha alijeruhiwa vibaya kutokana na vyupa vilivyokuwa vinavunjika kwenye magari hayo.

No comments:

 
 
Blogger Templates