Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kisarawe Beatrice Dominic akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkandarasi Ahmed Mussa wa Mohammed Limited Builders Limited wakuonesha mikataba waliyosaini ya ujenzi wa Kiwanda cha Korosho na aliyesimama katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe Zuberi Kizwezwe
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Tito Magoti pichani juu ametoa rai ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha Korosho Wilayani Kisarawe haraka iwezekanavyo.
Rai hiyo imetolewa na DC Magoti mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Kiwanda hicho cha Korosho ambapo pia alikua mgeni rasmi.
Aidha DC Magoti amemwambia Mkandarasi wa unenzi huo kuwa unjenzi ufanyike usiku na mchana ili msimu ujao wa Korosho wakulima wa Kisarawe wasihangaike kusafirisha korosho zao kupeleka Kibaha na Mkuranga kwa ajili ya kubanguliwa nakuwaongezea gharama wakulima kwa kukatwa fedha za ziada hivyo ujenzi wa Kiwanda hicho utawasaidia kupunguza gharama wakulima na baada ya ujenzi wataona faida ya zao hilo.
"Ujenzi wa Kiwanda hiki utaleta maendeleo ndani ya Kisarawe, Wilaya hii ipo kwa zaidi ya miaka 80 hatuna Hospitali kubwa,Kituo kikubwa cha Polisi,hatuna Idara ya Uhamiaji kwa kuona hilo Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amepanga kutuletea zaidi ya Bil.12 ambazo zitakuja kuleta maendeleo hivyo nawaasa wananchi na wote ambao mko kwenye maeneo ambayo fedha hizi za miradi mbalimbali zitapita nawaasa mziogope fedha za serikali na endapo itabainika unajishirikisha kuhujumu kuna kitu kinaitwa udava udava kitakukuta"amesema DC Magoti .
DC Magoti amesema hayo 18 Oktoba 2024 alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa jengo la kiwanda cha Korosho Kisarawe Mkoani Pwani.
Ujenzi wa Kiwanda hicho kitajengwa na Mohammed Builders Limited na kusinamiwa na Mkandarasi Ammar Janoowala kiwanda hicho kitajengwa kwa gharama ya Bi.2.5
Amesema kuwa Kiwanda hicho kitakua na uwezo wa kubangua tani 3 hadi 4 kwa siku moja na ujenzi huo unatarajiwa kuanza Novemba mosi mwaka huu
Mkandarasi Ahmed Mussa wa Kampuni ya Mohammed Builders Limited amesema kuwa anathibitisha ujenzi wa Kiwanda hicho utakamilika ndani ya mwaka mmoja.
Wakati huohuo DC Magoti amesema kuwa katika kukuza uchumi wa wakaazi wa Kisarawe pia watajenga soko la mihogo ili mkulima wa zao hilo aweze kufaidi na kuona matunda yake tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo wakulima wanauza bei kandamizi na za kinyonge wanazopangiwa na madalali
0 Comments