DC wa Kisarawe Petro Magoti akipokea kitenge ambacho ndiyo sare itakayovaliwa siku ya hafla ya Kisarawe Afya Gala itakayofanyika tarehe 2 Novemba 2024,akimkabidhi mjumbe wa Kamati Kisarawe Afya Gala Asia Mohammed.
Mkuu wa Wilaya Magoti ametoa wito kwa Viongozi ,wafanyabiashara wakulima na wadau mbalimbali wanaoishi ndani na nje ya nchi kujitokeza katika uchangishaji wa fedha za ujenzi wa jengo la VIP na ukarabati wa majengo ya Hospitali ya Kisarawe ambayo yamechakaa kwa sasa.
Mhe.Magoti amesema hayo jana 18,Oktoba alipozungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika ofisini kwake.
DC Magoti amesema kuwa hafla hiyo inafahamika kama Kisarawe Afya Gala imepangwa kufanyika tarehe 2 Novemba 2024 ambapo uchangishaji fedha utafanyika kwenye Ukumbi wa Minaki Sekondari uliopo Kisarawe.
"Nachukua fursa hii kuwakaribisha wadau wote katika Kisarawe Afya Gala ikiwa na lengo la kufanya harambee ya kuchangia fedha zitakazofanya ukarabati wa majengo yaliyochakaa na ujenzi wa jengo la VIP la kisasa labisa amesema "DC Magoti.
Aidha DC Magoti amesema kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya Kisarawe Afya Gala atakuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo pia wanatarajia kuwa na mgeni maalumu ambaye ni Waziri wa Afya Mhe.Jenista Mhagama.
Wakati huohuo DC Magoti katika kuchagiza Kisarawe Afya Gala amenunua kitenge ambacho ndiyo vazi maalumu siku hiyo kwa sh.100,000 na amesisitiza wadau wanunue ikiwa ni nji ya kuchangia hafla hiyo.
DC Magoti ametaja namba zinazopokea mchango kuwa ni Tigo 17403829 jina KISARAWE AFYA GALA na 21410007917 NMB.
Wakati huohuo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kisarawe Yonah Kabata amesema kuwa ujenzi hilo jengo utagarimu kiasi cha Mil.900 ambapo pia wamepanga jengo hilo la VIP lishabihiane na majengo ya Taasisi ya Jakaya Kikwete huku mgonjwa akiwa wodini apate huduma ya kiyoyozi ,
luninga na chakula.
"Katika Hospitali yetu tunatibu wagonjwa wengi hasa ikizingatiwa tuko karibu na mbuga ya Seluu watalii wanaokwenda huko pindi wakipata changamoto za afya wanaletwa hapa na wakiletwa wengi hushangaa hali ya uchakavu wa majengo yetu japo wengi wao huwa wako tayari kulipia gharama kiwango chochote cha fedha jambo ambalo limetupa msukumo wa kujenga jengo hilo la VIP la kisasa na kufanya ukarabati kwa majengo yote chakavu hospitalini hapa
DC Petro Magoti akimkabidhi kiasi cha Sh.100,000 ambayo ni malipo ya sare ya Kisarawe Afya Gala mwakilishi wa waratibu wa hafla hiyo itakayofanyika tarehe 2Novemba ,2024 anayepewa fedha hizo ni Mjunbe wa Kamati ya Kisarawe Afya Gala Bi Asia Mohammed.
0 Comments