Aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Michezo Tanzani Wakili Msomi Riziki Majala pichani juu amefariki dunia kwa kuuawa kutokana kudaiwa kupigwa na mtoto wake wa kwanza wa kiume aliyefahamika kwa jina la Juma Riziki Majala anayekadiriwa kuwa na umri kati ya (23na 24).
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mjumbe wa Mtaa wa Mkuza Kibaha Salumu Abasi Mtowela amesema kuwa mara baada ya kupata taarifa za tukio hilo leo 18 Oktoba 2024 majira ya asubuhi alikwenda kutoa taarifa Kituo kidogo Cha Polisi Kwa Matiasi alipofika Kituoni hapo tayari Polisi walishapata taarifa za mauaji ya Majala.
Aidha wakaondoka na Askari kwenda nyumbani kwa marehemu Majala na walipoingia ndani wamemkuta Juma akiwa amekaa pembeni ya mwili wa baba yake na nguo zilizokuwa na damu zikiwa zimewekwa kwenye ndoo hali iliyoashiria kwamba alipiga deki kufuta damu huku mwili wa marehemu ukiwa umelala chini sakafuni na ukivuja damu.
Polisi wamemchukua Juma na anashikiliwa na Kituo Cha Polisi Mjimdogo Kibaha Mkoani Pwani.
Wakati huohuo mpwa wa marehemu Wakili Msomi Majala aliyehitambulisha kwa majina ya Zuhura Salum Seif amesema yeye ndiye aliyezungumza na marehemu kwa mara ya amwisho jana usiku majira ya saa tatu na nusu ambapo mpwa huyo alimpigia mjomba wake ili wajadili mustakabali wa kesi yake ya mirathi ambayo marehemu Majala alikuwa Wakili wake amesema.
" Majira ya sa nne usiku 17,Oktoba ,2024 nilimpigia simu mjomba na tukawa tunajadili mwenendo wa kesi yangu ya mirathi ambayo iko Mahakama ya Temeke yeye ndiye alikuwa Wakili wangu ndipo nikasikia sauti ya Juma ambaye ni mtoto mkubwa wa mjomba anasema wewe mzee nipe pesa mimi nataka kwenda Bukene kwa sauti ya ukali baada yakusikia hayo maneno nikamwambia mjomba ampe simu niongee naye ili anipe namba nimtumie hiyo pesa anayohitaji sababu nilimsikia mjomba akimjibu kuwa haba pesa pia nikamsikia Juma akisema hataki kuongea na mtu yeyote yeye anataka pesa tu ndipo mjomba akaniambia nikate simu tutaongea baadaye au kesho na baada ya hapo leo asubuhi 18 Oktoba ,2024 nikakuta namba ya mjomba imenipigia niliipiga sana majira ya saa mojaasubuhi wakati huo mimi nilikua nje nilipoona hivyo nikapiga sana lakini haikuwa na majibu ndipo nikatuma ujumbe mfupi mmeamkaje huko mjomba nao haukujibiwa nikapiga tena sumu ndipo Juma akapokea simu akasema babake amefariki nikamuuliza ilikuwaje akasema,
yeye alitoka jana (17 ,Oktoba,2024) usiku alikwenda The Game Bar iko kwa Matiasi akarudi usiku alipofungua mlango ukawa mzito alipousukuma akakuta babake amefariki "niliposikia hivyo nikamwambia Juma kweli umemuua babako kwa sababu ya pesa akasema hajaua ndipo nilipowapigia ndugu zangu wanaoishi maeneo jirani na kwa mjomba nikawaambia waende kuhakikisha na walipofika wakanieleza hali halisi nimawaambia wasiingie ndani waende kutoa taarifa kituo cha Polisi, amesema Zuhura.
Wakati huohuo Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Pwani Muhudhwari Msuya anatarajia kutoa taarifa kamili ya tukio hilo kesho 19,Oktoba ,2024.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Tumbi Mkoa wa Pwani.
0 Comments