Meja Seif Hassan Kuwassa wa Kikosi Cha JKT Ruvu 832,Kilichopo Mlandizi Mkoani Pwani pichani juu akifurahia na Pundamilia.kwenye bustani hiyo.
Uongozi wa Bustani ya wanyamapori ya JKT Ruvu 832 iliyopo Mlandizi Kibaha Mkoani Pwani umejipanga kumleta mfalme wa nyika Simba ikiwa ni katika kuiongezea hadhi bustani hiyo.
Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari hivi karibuni katika mkutano uliofanyika kwenye bustani hiyo Meja Seif Hassan Kuwassa amesema kuwa bustani hiyo yenye ukubwa wa heka 70 imezinduliwa mwezi Mei mwaka huu huku ikiwa imejengewa uzio yenye wanayamapori aina saba kwa sasa lakini hivi karibuni tumejipanga kumleta Simba ambaye atafugwa kwenye banda maalumu tofauti na ilivyo kwa wanyamapori waliopo hivi sasa ambao wamekua wakitembea kwa uhuru kama mnavyoona amesema Meja Kuwassa.
Aidha Meja Kuwassa ametaja aina ya wanyamapori wanaopatikana hivi sasa kwenye bustani hiyo ya 'Ruvu Wildlife' kuwa ni Twiga, Pofu,Pundamilia,Swala aina mbili Impala na Pongo,Nyumbu na ndege wa aina mbili Mbuni asiyeruka na Korongo.
Amesema kuwa wanyama hao ambao ukifika wanaonekana wakiwa wanatembea bila kizuizi chochote wamepatiwa mafunzo ya kuishi na binadamu hivyo hawana madhara.
"Kabla ya kuachiwa kweye bustani wanyamapori hawa wamepatiwa mafunzo na mtaalamu wa wanyamapori ndiyo maana wanaishi kiraafiki hata wakiona watu wanawafuata bila ya uoga wa aina yeyote, mtalii akifika kuna maelekezo atapatiwa na wataalamu wetu hivyo atakuwa huru kuwalisha chakula maalumu na kupiga nao picha kwa karibu" amesema Meja Kuwassa.
Meja Kuwassa amezungumza kwa niaba ya Mkuu wa Kikosi Cha JKT Ruvu 832 Kanali Peter Elius Mnyani, ambaye ndiye aliyetoa wazo la kuanzishwa kwa mradi huo ameongeza kwa kusema kuwa kuna wanyama wengine ambao wanapatiwa mafunzo na baada ya miezi sita watawaachia kwenye bustani hivyo idadi ya wanyama hao itaongezeka na kuleta kivutio zaidi.
"Wazo la kuanzishwa kwa bustani hii limetoka kwa Kanali Mnyani akalifikisha kwenye bodi likapita bila kupingwa na kuzinduliwa mwezi Mei 2024 " amesema Meja Kuwassa.
"Mradi huu una lengo la kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan jinsi anavyoitangaza nchi kwa kupitia utalii ndani na nje ya nchi hivyo nasi tumeamua kuutangaza utalii wa ndani amesisitiza Meja Kuwassa.
Baadhi ya wanyamapori wakijivinjari kwenye bustani ya 'Ruvu JKT Wildlife' iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani
Meja Kuwassa amesema kuwa tangu bustani ilipozinduliwa muitikio wake unaridhisha kwani hupata watalii wa nje saba ndani ya juma na mwishoni mwa wiki familia mbalimbali huenda kubarizi katika bustani hiyo.
Amesema kuwa huduma zingine zinazopatikana ni pamoja na kuwa na mabwawa ya kuogelea kwa wakubwa na watoto, kadhalika kuna michezo mbalimbali ya watoto kama kuendesha gari ,baiskeli inapatikana,
chakula kinapatikana pamoja na
vinywaji aina zote.
Meja Kuwassa ametoa wito kwa wakaazi wa maeneo ya Mlandizi na viunga vya jirani ndani na nje ya Mkoa wa Pwani ambao hawajawahi kwenda mbugani kuona wanyamapori wanakaribishwa 'Ruvu Wildlife' wakajionee wanyama kwa uhalisia kwa sababu panafikika kwa urahisi ni mkabala na barabara ya Morogoro na kuna mandhari nzuri kwa ujumla.
"Huu mradi unajitegemea na tumefuata taratibu zote zinazohusu Wanyamapori" amesema Meja Kuwassa.
Baadhi ya wanyamapori akiwamo Twiga wakijivinjari kwenye bustani ya 'Ruvu JKT Wildlife' iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani
Meja Seif Hassan Kuwassa wa Kikosi Cha JKT Ruvu 832,Kilichopo Mlandizi Mkoani Pwani akifafanua jambo kwenye Mkutano na na Waandishi wa Habari hawapo pichanai kwenye mkutano uliofanyika kwenye bustani hiyo .
Kutoka kushoto ni Meja Seif Hassan Kuwassa na Mtaalamu wa wanyamapori wa 'Ruvu Wildlife 'Ezekiel Mollel wakizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani.
Pichani ni Mtaalamu wa wanyamapori na.mkufunzi wao Ezekiel Mollel.
Kutoka kushoto ni Meja Seif Hassan Kuwassa akiwa na Mtaalamu wa wanyamapori wa 'Ruvu Wildlife 'Ezekiel Mollel wakizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani.
Mtaalamu na Mkufunzi wa Wanayapori Ezekiel Mollel amesema kuwa kuna faida ya kwenda mbugani ama bustani ya wanyamapori unaondoa sonona na kuleta afya ya akili.
"Binafsi nina utaalamu wa kongea na wanyama hivyo wakifika hapa wanafungiwa na kupatiwa mafunzo ndani ya miezi sita ndipo wanaachiwa huru kwrnye bustani kama mnavyoona hawana madhara kwa binadamu,wakiona watu wanawafuata kama wanawakaribisha mazingira ya hapa Ruvu ni rafiki kwao wanajiona kama wako mbugani pana rutuba majani yanamea wanakula na hivi vyakula tunavyowapa ni maalumu nikama vitafunywa mbavyo ndivyo watalii wakija tunawapa wawalishe haturuhusu mtu kuingia na chakula au kumpa mnyama kitu chochote cha tofauti" amesema Mollel.
"Kiingilio ni 50,000 kwa mkubwa mtoto 30,000 pia tunazo bei za wanafunzi wa vyuo pia tunaruhusu watu kuja kusherehekea siku zao za kuzaliwa na Pre Wedding.
ReplyForward |
0 Comments