Mbunge wa viti maalum mkoa
wa Iringa Ritta Kabati (CCM) akimkabidhi mwenyekiti wa waandishi wa habari mkoani Iringa moja ya jezi alizotoa kwa waandishi wa habari kwa ajili ya mechi mbalimbali za timu hiyo
Mbunge wa viti maalum mkoa
wa Iringa Ritta Kabati (CCM) ameipiga jeki timu ya wandishi wa habari
mkoa wa Iringa kwa kuwapatia jezi seti moja ,mpira na
pesa taslim kiasi cha Tsh 50O,000 ili viwasaidie katika malengo yao
ya kukipiga ligi daraja la kwanza .
na fredy mgunda,Iringa
Mbunge wa viti maalum mkoa
wa Iringa Ritta Kabati (CCM) ameipiga jeki timu ya wandishi wa habari
mkoa wa Iringa kwa kuwapatia jezi seti moja ,mpira na
pesa taslim kiasi cha Tsh 50O,000 ili viwasaidie katika malengo yao
ya kukipiga ligi daraja la kwanza .
Akikabidhi
msaada huo kwa mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari mkoa wa Iringa
Frank Leonard juzi mbunge huyo
alisema kuwa yeye kama mlezi wa timu hiyo ameamu kujingiza kwa miguu yote
kuisaidi timu hiyo ambayo inaonekana kufanya vema kwenye mchezo wa soka mkoani
hapo .
Kabati alisema kuwa licha ya kuwa mpira ni ajira pia
unamsaidia mtu kuwa na afya njema itakayomsaidia kujiepusha na magonjwa yanayoepukika
ikiwemo presha .
“Niwatie moyo hichi mulichokianzisha ni kizuri na timu yenu
ina fanya vizuri na juzi tu mumenyakua kombe la Spanest kwa kuwanyuka kitisi huu ni ushahidi tosha
mukiendelea hivi hivi mutakuja kuingia ligi daraja la kwanza na baadaye ligi
kuu .
Kabati aliwataka wadau wengine
mkoa Iringa na nje ya Iringa kuendelea kujitolea
kuisaidia timu hiyo ya
wanahabari ili iendele kufanya vema ndani na nje ya mkoa wa iringa
Akipokea vifaa hivyo mwenyekiti wa wanahabari mkoa wa Iringa
Frank Leonard alimshukuru mbunge huyo kwa vifaa na fedha alizotoa huku
akimuahidi mbunge huyo kuwa timu hiyo itakipiga na timu mbalimbali ikiwemo timu
ya bunge la jamuhuri wa muungano wa Tanzania
Frank alisema kuwa timu hiyo imekuwa ikifanya vema kutokana
na kuwa na wandishi wazuri vijana waliona ari ya kusakata kambumbi hivyo ni
vema timu ya bunge kujipanga kisawasa kwani hawata toka salama pindi
watakapokipiga nao mjini dodoma.
0 Comments