Akizungumza mbele ya Wanahabari mapema leo (hawapo pichani) ndani ya Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO,Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN),Joachim Mushi amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 5 na 6 ,2016 hapa hapa jijini Dar,ambao utawashirikisha wanachama wapatao 150 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.Mushi alisema kuwa katika mkutano huo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari,Sanaa,Michezo na Utamaduni ,Mh Nape Mosses Nnauye,
"Mgeni rasmi anaetarajiwa kufungua mkutano huo ni Waziri Nape Nnauye,lengo kuu la mkutano huo likiwa ni kupeana elimu na kubadilishana mawazo juu ya uendeshaji wa Mitandao ya Kijamii kwa manufaa,upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuzingatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji",alisema Mushi.
Alisema kuwa uendeshaji wa Mitandao baadhi yao wanaifanya ni kama ajira nyingine,hivyo kimsingi lazima wakubali kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la kusambaza habari mbalimbali tena kwa muda mfupi tangu kutokea kwa tukio fulani,hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwapiga msasa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya ya mitandao hii,
Mkutano huo utakaokuwa wa aina yake na kuiandika historia tangu kuanza kwa mitandano ya Kijamii hapa nchini,umedhaminiwa na Benki ya NMB ambaye ni mdhamini mkuu ,NHIF, SBL, PSPF na Coca Cola
0 Comments