Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Mbeya Sambwee Shitambala
Na
Mwandishi wetu,Mbeya
KESI ya kuingia kwa jinai inayomkabili mgombea ubunge kupitia chama cha
mapinduzi Jimbo la Mbeya mjini, Sambwee Shitambala, imeendelea kusikilizwa leo
katika Mahakama ya Wilaya ya Mbeya.
Shitambala ambaye ni Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, anatuhumiwa kwa kosa la kuingia kwa jinai baada ya kuvamia na kujenga kwenye eneo la mtu kinyume na sheria katika kiwanja kilichopo eneo la Gombe Jijini hapa.
Kosa hilo ni kinyume cha sheria ya 266(a) sura ya 16
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 .
Akisomewa
shitaka hilo na Mwendesha mashitaka wa serikali, Wakili Baraka Mgaya, mbele ya
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Girbelt Ndeuluo, alisema
mtuhumiwa alitenda kosa hilo kati ya Juni, 2012 na February 2013 katika eneo la
Gombe lililopo Jijini Mbeya
Alisema,
mtuhumiwa aliingia kwenye eneo la ardhi kiwanja namba 27 na 28 kilichopo katika
eneo la Block Bb kata ya Itezi Jijini hapa,mali ya Jaswinda Palsin(Singa Singa)
ambaye ni raia kutoka bara la Asia na kujenga nyumba yake ya makazi kitendo
kinachodaiwa kuwa ni kumfanyia maudhi raia huyo.
Hakimu
Ndeuro, aliihairisha kesi hiyo hadi September 15, mwaka huu, ambapo upande wa
mashitaka utakapoleta watuhumiwa wengine
wanne watakaoungana na Shitambala kujibu tuhuma zinazowakabili za
kuingia kwa jinai kwenye eneo la kiwanja cha Singa Singa huyo.
Hata hivyo
taarifa za kuaminika zilizoifikia Blog hii zimeeleza kwamba mgombea huyo pia
amevuliwa wadhifa wake wa uwakili kutokana na kuendesha shughuli za kiwakali zaidi ya miaka mitatu bila ya kulipa kodi ya
serikali ambayo ni kinyume cha utaratibu na ukiukwaji wa sheria za maadili
katika utumishi wa umma.
0 Comments