Monica Mbega akimwombea kura mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini leo |
Monica Mbega akimpongeza Mwakalebela |
Monica Mbega akijiandaa kumsalimia Kiponza |
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Bw Abeid Kiponza (kulia) akimtambulisha mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela leo |
Mwakalebela akizungumza na wana CCM leo |
Mgombea udiwani wa kata ya Mtwivila Bw Jose Mgongolwa (kulia) akitambulishwa na Mwakalebela |
Mgombea udiwani Bw Chatanda kulia akitambulishwa na Mwakalebela |
Mwakalebela akimtambulisha Ibrahim Ngwada (kulia) mgombea udiwani kata ya Mshindo |
Mgombea udiwani wa kata ya Mvinjeni akitambulishwa |
Mgombea udiwani wa kata ya Mkimbizi Bi Farida Mpogole akitambulishwa na Mwakalebela |
Mwakalebela akimtambulisha mgombea udiwani wa kata ya Gangilonga Bw Nicholina Lulandala |
Mwakalebela akimtambulisha mgombea udiwani wa Kwakilosa Bw Himid Mbata (kulia) |
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Bw Abeid Kiponza akimtambulisha mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia CCM Bw Frederick Mwakalebela (kushoto)
...............................................................................................................................
Na MatukiodaimaBLog
ALIYEKUWA
mmoja kati ya wagombea wa nafasi ya urais kupitia chama cha
mapinduzi (CCM) na mbunge wa zamani wa jimbo la Iringa mjini Bi
Monica Mbega amesema kuwa mbali ya kuwa yeye alikuwa ni mmoja kati
ya walioomba kuteuliwa kuwania nafasi ya urais na jina lake kukatwa
bado hana kinyongo na mteuliwa wa CCM Dr John Magufuli kwani
anamkubali kwa asilimia 100 kuwa ni chaguo la watanzania kama ilivyo
kwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Iringa mjini Bw Frederick
Mwakalebela .
Mbega
ambae alikuwa ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini kwa vipindi
viwili kati ya mwaka 2000 -2010 alitoa kauli hiyo leo wakati
akizungumza na wanachama wa CCM katika viwanja vya CCM wilaya ya
Iringa mjini wakati wa mgombea mteule wa ubunge jimbo hilo la Iringa
mjini Bw Mwakalebela kutoka kuchukua fomu kwa msimamizi mkuu wa
uchaguzi jimbo la Iringa mjini kwa ajili ya kuwania ubunge kupitia
CCM.
Alisema
kuwa katika mchakato wa ndani ya chama wa kuwania kuteuliwa
kugombea Urais yeye alikuwa ni kati ya wanachama zaidi ya 40
waliojitokeza kuchukua fomu akiwemo Dr Magufuli na kuwa baada ya
vikao vya juu vya chama kukamilisha taratibu za kumpata mgombea
mmoja hakuwa na kinyongo cha kuhama chama wala kukaa nyuma katika
mambo ya chama na ndio maana ameamua kurejea nyumbani kwake ili
kuungana na wana CCM kurejesha jimbo hilo kwa CCM na kuwapigia
kampeni wagombea wote wa CCM akiwemo mgombea wa nafasi ya urais Dr
Magufuli na madiwani pia.
"Kweli
nawapongeza sana wananchi wa Iringa mlinipa udhamini wa kutosha
wakati wa mchakato wa kuomba kuteuliwa kuwa mgombea Urais wa CCM
nilipata watu 45 kati ya 35 waliokuwa wakihitajika kweli ni watu
wengi sana na baada ya mchakato jina langu halikupitishwa na jina la
mwenzetu Dr Magufuli ndie aliyeteuliwa na kazi yetu ni kumuunga mkono
kwani kati ya watu wote 41 ni nafasi mmoja pekee ndio ilitakiwa
....hivyo hakuna haja ya kuwa na kinyongo kwa kuhama chama chetu "
Mbega
aliwataka wana CCM jimbo la Iringa mjini kuweza kuunganisha nguvu
zao kwa mgombea ubunge Bw Mwakalebela ili kuweza kulikomboa jimbo
hilo na kuhakikisha mgombea Urais na madiwani wa CCM wanapata kura
za kishindo zaidi katika jimbo la Iringa mjini .
Alisema
kwa wanachama wa CCM ambao waligombea nafasi mbali mbali na kura
kutotosha katika nafasi walizoomba wanapaswa kuvunja makundi yao na
kuunganisha nguvu zao kwa wale walioshinda ili kufanya kazi ya
kujenga chama badala ya mtu .
Hata
hivyo alisema kwa upande wake atapambana kwa nguvu zote kuhakikisha
chama kinapata ushindi mkubwa katika jimbo hilo la Iringa mjini na
kudai kuwa kazi kubwa iliyopo mbele kwa wana CCM ni kujenga
utamaduni wa kusamehe na kusonga mbele.
Katibu
wa CCM wilaya ya Iringa mjini Elisha Mwampashi akimkaribisha
mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Bw Abeid Kiponza
kumtambulisha rasmi mgombea ubunge wa jimbo hilo ,alisema kuwa ni
lazima watanzania na wananchi wa jimbo la Iringa mjini kuwapuuza
wale wote wanaohama CCM mara baada ya kushindwa katika kura za
maoni na kuwa watu hao hawana mapenzi mema na Taifa bali wapo kwa
ajili ya maslahi yao zaidi .
Mwampashi
alisema kuwa kinachoshangaza ni kuona UKAWA ambao walikuwa mbele
kupinga vitendo vya ufisadi na kumtuhumu wazi wazi waziri mkuu
mstaafu Edward Lowasa kuwa si mtu msafi leo wamempokea na kuwa
mgombea wao wa nafasi ya urais jambo ambalo watanzania wanapaswa
kujiuliza juu ya mwenendo wa UKAWA katika Taifa hili.
Mwenyekiti
wa CCM Iringa mjini Bw Kiponza alisema kuwa kazi kubwa ya CCM jimbo
la Iringa mjini ni kulikomboa jimbo hilo kutoka kwa aliyekuwa mbunge
wa jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa (chadema) ambae hakuna
maendeleo yoyote aliyoyaleta katika jimbo hilo kwa kipindi chote
cha miaka mitano zaidi ya wana Iringa kusababishiwa kupigwa mabomu na
lugha zisizofaa majukwaani .
Hivyo
alisema wana Iringa wanayosababu ya kusema basi kuendelea kukosa
maendeleo na kufanya maamuzi sahihi ya kukirejesha chama cha
mapinduzi madarakani kwa kumchagua mchapa kazi Bw Mwakalebela ambae
kwa muda wake mfupi wa ukuu wa wilaya ya wanging'ombe kazi kubwa
amepata kuionyesha na hivyo ni zamu ya wana Iringa kushuhudia
maendeleo hayo kwa kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo .
"
Toka ameondoka Mbega mwaka 2010 kwa kuanzisha miradi ya barabara
na maji ya JR hakuna mradi ulioendelea chini ya ubunge wa Msigwa
zaidi ya maandamano na mabomu kila wakati na kupinga wananchi
kushiriki katika shughuli za kimaendeleo"
Kwa
upande wake mgombea huyo wa ubunge jimbo la Iringa mjini Bw
Mwakalebela alisema kuwa chini ya ilani ya CCM serikali imefanikiwa
kuleta maendeleo kila kona ya nchi hii na hadi sasa wapo wanaopinga
kuwa akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa ila ukweli upo wazi
kwa wana Iringa kuona kasi kubwa ya miradi ya maendeleo iliyoletwa
na CCM inayoongozwa na wenye akili ndogo kama mbunge wa jimbo hilo
anavyojinasibu majukwaani na kuwa haja ya wananchi kumhoji mwenye akili
kubwa ni ahadi gani aliyoahidi ambayo amepata kuwatimizia wananchi
wake .
Mwakalebela
alisema kuwa ni wakati mzuri kwa wana Iringa kupima akili ndogo na
kubwa katika maendeleo na sio katika majukwa ya siasa na mwisho wa
siku shughuli za maendeleo zinasimama na wananchi kushuhudia
maandamano kila uchwao .
Alisema
kuwa iwapo wananchi wa Iringa watamchagua kuwa mbunge wa jimbo
hilo Octoba 25 mwaka huu wawe na matumaini mapya ya kimaendeleo
ikiwa ni pamoja na kuanzisha mfumo mzuri wa kuwakomboa wanawake na
vijana kiuchumi kwa kuwapa mikopo nafuu.
0 Comments