Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela, aliyefariki usiku wa kuamkia leo wakati alipofika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Afrika ya Kusini zilizopo Masaki jijini Dar es salaam leo. Mzee Nelson Mandela (95) alifariki Dunia jana usiku nyumbani kwake Houghton, Jouhannesburg. Kushoto ni Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini, Henry Thanduyise Chilize.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitoa heshima za mwisho mbele ya picha ya marehemu Nelson Mandera
baada ya kusaini kitabu cha maombolezo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini Tanzania, Henry Thanduyise Chiliza (kulia) na baadhi ya Viongozi wa
Ubalozi huo kwenye ofisi za Ubalozi wa Afrika ya kusini Masaki jijini
Dar es salaam leo, baada ya kusaini kitabu cha maombolezo.
0 Comments