Pichani
kati ni Miss Earth Tanzania 2012,Bahati Chando akizungumza mbele ya
Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo kwenye hoteli ya Lamada,Ilala
jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa sherehe yao ya "Mother's Day", siku
ya Mama Duniani itakayofanyika Mei 12,2013 kwenye hoteli hiyo, ambapo
kauli mbiu ya Mwaka huu imepangwa kuwa ni "always in our heart's",
"tukiwakumbusha akina mama zetu kwamba wapo moyoni mwetu na tunawapenda
sana" alisema Chando.
Shoto ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa na kulia ni Mratibu wa hafla hiyo, Bi.Regina Ogwalla. Bahati amesema kuwa katika hafla hiyo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Mwenyekiti wa UWT Ilala,Mh.Nora Mzeru.
Shoto ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa na kulia ni Mratibu wa hafla hiyo, Bi.Regina Ogwalla. Bahati amesema kuwa katika hafla hiyo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Mwenyekiti wa UWT Ilala,Mh.Nora Mzeru.
Miss
Earth Tanzania 2012,Bahati Chando amesema kuwa ameamua kuungana na
Diwani wa kata ya Kipawa, Mh. Bonnah Kaluwa kuandaa hafla hiyo
itakayozinduliwa na Wamama wa Ilala,kutambua umuhimu wa kina
mama,kuwafurahisha lakini pia kuwaelimisha kuhusu mambo
mbalimbali,amesema kuwa amekuwa na shauku kubwa ya kuandaa sherehe kama
hiyo ili kujitoa na kusaidia watu kama watu wengi walivyoungana
kumsaidia katika safari yake ya kuwa mrembo wa kupeperusha bendera ya
Tanzania Kimataifa.
Pia
anasema kuwa ameandaa sherehe hiyo kuonyesha jamii kwamba,kuwa mrembo au
miss sio tu kupozi mbele ya Kamera,bali inaambatana na na jukumu la
kugusa jamii kwa namna mbalimbali.
Shoto ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa akitoa ufafanuzi kuhusiana na uzinduzi wa sherehe yao ya "Mother's Day",siku ya Mama Duniani itakayofanyika Mei 12,2013 kwenye hoteli hiyo,ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu kwenye hafla hiyo umepangwa kuwa ni "always in our heart's", |
0 Comments