SHIRIKISHO la Ngumi la Kimataifa (IBF) limempongeza bondia maarufu wa kitanzania Francis Cheka kwa juhudi zake za kuwa bondia mzuri mwenye viwango vya kimataifa katika uzito wa Super Middleweight.
Francis Cheka aliweza kutetea mkanda wake wa IBF Africa uzito wa Super Middle baada ya kumshinda kwa KO
bondia Thomas Mashali aka “Simba asiyefugika” tarehe 1 Mei, 2013
katika ukumbi wa PTA jijini Dar Es Salaam.
IBF inachukua fursa ya
kumpongeza Francis Cheka baada ya
ushindi huo ambao umedhihirisha kuwa yeye
kweli ni bingwa wa bara la Afrika. Francis Cheka atarudiana na bondia wa Malawi
Chimwemwe Chiotcha mwezi wa Agusti katika mpambano la kutetea
mkanda wake.
Mpambano wao wa
marudiano utafanyika katika jiji la Blantyre
nchini Malawi na tayari
majadiliano ya mpambano huo yanaendelea vizuri. Kampuni ya “Mawenzi Boxing Promotion” ya nchini Malawi chini ya bwana Stephen Mawezni ndiyoitakayoandaa
mpambano huo.
Pambano hili linakuja
baada ya wadau kadhaa wa ngumi kuomba mabondia hao warudiane walipoonyesha ujuzi
mkubwa na ushindani katika mpambano wao Desemba
26 mwaka jana katika uwanja wa Sheikh
Amri Abeidi jijini Arusha siku ya Boxing
Day.
Baada ya mpambano huo,
IBF itampatia Francis Cheka nafasi
ya kugombea mkanda wa IBF wa Kimataifa (IBF
International Super Middleweight) na mabondia wa Ulaya au Marekani. Hii ni kudhihirisha kuwa Francis Cheka hana tena mpinzanai nchini Tanzania na kumpambanisha
na mabondia wa kitanzania ni kumpotezea muda na uwezekano wake wa kutengeneza
jina na pesa.
Wakati huo huo bondia Thomas
Mashali bado ni bingwa wa Afrika ya
Mashariki na Kati (ECAPBF) katika uzito wa Middle kwani mkanda wake haukuwa kati ya mikanda iliyogombewa
kwenye mpambano uliomalizika Mei mosi.
0 Comments