Social Icons

Saturday, April 1, 2017

KILI FM INTERNATIONAL TOURISM MARATHON KUTIMUA VUMBI AGOSTI 2017
Mratibu Kili FM Half Marathon  Nelson Mrashani akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani.


Mwenyekiti wa Kili FM  Sports Club  Ewala  Masakuya Lekule  akizungumza kuhusu mbio hizo.(Picha zote na MAELEZO).

Uongozi wa Kili FM  Half Marathon umetangaza leo kwamba mbio hizo za Kimataifa zimepangwa kufanyika Agosti 13 mwaka huu Mkoani Kilimanjaro ambapo wanatarajia kusajili wakimbiaji 5,000.

Akizungumza leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO  Jijini Dar  ea Salaam  Mwenyekiti wa Kili FM Sports  Club Ewala  Masakuya  Lekule alisema katika mbuo hizo za mwaka huu kutakuwa na kauli mbiu tatu amnazo ni utunzaji wa mazingira , kupinga mauaji ya albino na mauaji ya Tembo.

Alisema  washindi katika mbio hizo watapata zawadi za fedha taslim  na medali.Pia wameahidi kutoa msaada kwenye vituo vya vya kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi Albino.

Mwisho amemaliza kwa kuomba sapoti kutoka kwa  wadau mbalimbali kutoa udhamini.

No comments:

 
 
Blogger Templates